Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA Aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga Kiwanda cha Chai cha Kilolo?

Supplementary Question 1

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninachukua nafasi hii kuishukuru sana Serikali kwa kuvutia wawekezaji walioweza kujenga kiwanda kile. Ni ukombozi mkubwa sana kwa Wana-Kilolo. Pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kiwanda hiki ulitakiwa uende sambamba na ujenzi wa kiwanda cha sukari ambacho kinatengenezwa na watu wa TEMDO. Sasa ni lini Serikali itapeleka mitambo ya kuchakata sukari ili iweze kusimikwa katika eneo ambalo lilishaoneshwa pale Mahenge kama ambavyo ilikuwa ahadi ya Serikali na Wizara hii kwenye bajeti ya mwaka jana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Wilaya ya Kilolo ni wazalishaji wakubwa sana wa matunda lakini matunda mengi yanaoza kutokana na kwamba hakuna kiwanda kinachoweza kuyachakata.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuvutia uwekezaji wa angalau kiwanda kimoja kwa ajili ya kuchakata matunda ili kuongeza thamani na kuwafanya Wananchi wa Kilolo waweze kunufaika?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, kwanza, ninachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Justin Nyamoga kwa kazi kubwa nayofanya kufuatilia na kuhakikisha hiki kiwanda kinajengwa pale Kilolo maana kilikuwa ni kilio cha Wana-Kilolo kwa muda mrefu baada ya yale mashamba ya chai ambayo yalikuwa yametelekezwa na sasa haya ni matokeo ya ufuatiliaji wa Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maswali yake mawili ya nyongeza; Serikali inatekeleza ahadi zake na ndiyo maana hata ujenzi huu wa kiwanda hiki cha chai ni utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Serikali kutipitia bajeti tunayokamilisha mwaka huu wa fedha wa 2024/2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye suala la Kiwanda cha Sukari pale Mahenge, ninajua wakulima tayari nao wameshalima miwa kama ambavyo kwenye chai kule Kilolo. Kwa hiyo, tunawahakikishia katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2025/2026, tumeweka bajeti hiyo kwa ajili ya kukamilisha kiwanga kile kinachosanifiwa na TEMDO na kitaenda kufunga pale Mahenge ili na wao pia waweze kunufaika na uwepo wa miundombinu hii wezeshi ya viwanda ambayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshasisitiza kuhakikisha sekta binafsi inakuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, ni kweli Kilolo ni moja ya maeneo ambayo yanalima mazao mengi ikiwemo matunda, chai na mbogamboga. Tayari Serikali ina mpango mahsusi wa kuendeleza sekta ya matunda na mbogamboga na tayari Kilolo, pale Ilula kuna kiwanda kile cha Dabaga ambacho kinachakata nyanya ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno. Hali kadharika tutaenda kufanya kazi kuhakikisha tunaleta viwanda vingine zaidi vya kuongeza thamani matunda kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge umesema ili kupunguza upotevu wa matunda ambayo yanakosa kuongezwa thamani ili kuendeleza sekta ya kilimo na matunda katika Jimbo la Kilolo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA Aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga Kiwanda cha Chai cha Kilolo?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga kiwanda cha kuchakata madini ya chumvi katika Mji Mdogo wa Nangurukuru ili kuwasaidia wazalishaji wa chumvi wa Mkoa wa Lindi? (Makofi)

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, kwanza na mimi ninachukua nafasi kumpongeza Mheshimiwa Ndulane kwa kufuatilia sekta hii ya chumvi kule Lindi na mahsusi kule Kilwa, Nangurukuru na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuvutia wawekezaji na tayari tunao wawekezaji wengine wameshaonesha nia ikiwemo wa ndani pamoja na taasisi zetu ikiwemo Magereza ambao wanaendelea kuchakata chumvi ili kuongeza kipato na thamani ya madini haya ya chumvi katika maeneo tofauti ikiwemo kwa Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, na kwake tutaendelea kuvutia wawekezaji ili waje pale Nangurukuru ili kuweka viwanda hivyo vya kuongeza thamani ya chumvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA Aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga Kiwanda cha Chai cha Kilolo?

Supplementary Question 3

MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kile Kiwanda cha MUTEX - Musoma Serikali ilipokibinafsisha kwa private sector, haikuweza kuwalipa wale wananchi au watumishi mafao yao.

Je, ni lini sasa Serikali itatimiza hiyo adhima ya kuwalipa ili waweze kuendelea na maisha yao? (Makofi)

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, pia ninampongeza Mheshimiwa Vedastus Manyinyi kwa sababu naye amekuwa akifuatilia sana pamoja na viwanda vingine lakini hiki Kiwanda cha MUTEX. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya maeneo ambayo Serikali imeweka msisitizo ni kuona namna gani moja, kuona namna ya kufufua viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo vimetelekezwa na wawekezaji hawa, laikini pili, kuangalia mafao ya wale watumishi au waliokuwa wafanyakazi kwenye viwanda hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inalifanyia kazi, kuona wale ambao walikuwa na madai kwenye viwanda hivi ambavyo vilibinafsishwa na havijaendelezwa ili wapete haki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tuhakikishe ni namna gani ya kufufua viwanda hivyo ili viendelee kutoa ajira na kuongeza thamani na malengo ya kiwanda kama MUTEX kwenye sekta ya pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.