Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Water and Irrigation Wizara ya Maji 273 2025-05-09

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO Aliuliza: -

Je, lini usambazaji wa maji ya Ziwa Victoria katika Kata za Mondo, Busangwa, Sekebugolo na Mwasubi - Kishapu utakamilika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa mradi wa kutumia maji ya Ziwa Victoria kwenda kwenye Kata za Wilaya ya Kishapu ikiwemo Kata za Mondo, Busangwa, Sekebugolo na Mwasubi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la mradi huo ni kutatua changamoto ya huduma ya maji katika kata hizo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 16.1 kinahitajika. Kwa sasa Serikali inaendelea na utafutaji wa fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo. Aidha, kwa sasa huduma ya maji inapatikana kwa baadhi ya maeneo ya kata hizo kupitia visima vya pampu za mkono 12, Bwawa la Sekeididi pamoja na mtandao wa mabomba wa zamani.