Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 10 | Finance | Wizara ya Fedha | 122 | 2025-04-23 |
Name
Constantine John Kanyasu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita Mjini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:-
Je, nini hasara na faida kwa kampuni kutotekeleza Sheria ya kujiorodhesha kwenye Dar es Salaam Stock Exchange?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria ni makampuni ya simu pekee ndio hulazimika kuuza hisa kwa umma na kuorodheshwa katika soko la hisa isipokuwa yale makampuni ambayo Serikali ina umiliki wa hisa kwa 25% au zaidi na makampuni ambayo yanatoa huduma ya minara ya simu.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kampuni kujiorodhesha kwenye soko la hisa kuna faida lukuki ikiwa ni pamoja na: kuongeza mtaji, kuongeza ufanisi na tija, kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki, kutambua thamani halisi ya hisa zake ambapo wanahisa watapata thamani ya hisa zao wanapotaka kuuza kwa kufuata mwenendo wa soko yaani demand and supply, kuwapa wananchi fursa ya kununua hisa na hivyo kuwezeshwa kushiriki katika uchumi wa nchi. Aidha, soko la hisa pia hutoa fursa kwa wawekezaji wanaotaka kuuza uwekezaji wao kipindi wanapohitaji fedha.
Mheshimiwa Spika, wanahisa wa kampuni ambayo haijaorodheshwa katika soko la hisa hukutana na changamoto za kutofahamu thamani halisi ya uwekezaji walioufanya kutokana na kukosekana kwa ukwasi wa hisa zao. Kampuni hizi hutawaliwa na kukosekana kwa uwazi na hivyo Serikali na wanahisa kushindwa kupata taarifa stahiki za mwenendo wa biashara na fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved