Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:- Je, nini hasara na faida kwa kampuni kutotekeleza Sheria ya kujiorodhesha kwenye Dar es Salaam Stock Exchange?
Supplementary Question 1
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu haya mazuri ya Serikali ninayo maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kampuni za madini mathalani Geita Gold Mine (GGM), Barrick pamoja Shanta mine, zinaaminika kuwepo katika masoko ya hisa ya nje. Kama tulipitisha sheria hapa kwamba Serikali inapaswa kuwa na 16% ya share as free carried interest. Ni lini Serikali itasema ni lazima kampuni hizi kuwepo katika Dar es Salaam Stock Exchange Market?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Soko la Hisa linatoa taswira ya Kampuni zinazofanya vizuri kwa namna ya watu wanavyonunua na kuuza. Je, Serikali sasa haioni haja ya kubadili sheria ili iwe ni lazima kwa kampuni zote kubwa kujiunga? (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abeid kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ninaomba uridhie nijibu maswali yote mawili kwa pamoja kwa sababu yote yanahusu mabadiliko ya sheria. Tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, tunaenda kuufanyia kazi na wadau wa sheria tunawajua likiwa ni pamoja na Bunge lako Tukufu. Kwa hiyo, tukiona kwamba jambo hili litakuwa na tija kwenye kubadilisha sheria hiyo basi Serikali haitosita kulifanyia kazi na kuleta hapa katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved