Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 10 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 123 2025-04-23

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-

Je, SIDO ina mpango gani kukopesha Wajasiriamali vifungashio kama ambavyo benki zinavyokopesha fedha ili kuongeza ubora wa bidhaa?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ajliibu:-

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Serikali kupitia SIDO huwarahisishia Wajasiriamali kupata vifungashio kwa kununua kwa jumla (bulk procurement) na Wajasiriamali kuweza kupata vifungashio hivyo katika ofisi za SIDO mikoani kwa kuuziwa rejareja na kwa bei nafuu. Utaratibu huo umewawezesha Wajasiriamali kupata vifungashio kwa wakati na kwa kutumia mikopo ya NEDF inayotolewa na SIDO.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa vifungashio kwa wajasiriamali, Serikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya vifungashio hapa nchini ili kurahisisha upatikanaji wake na kwa bei nafuu. (Makofi)