Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, SIDO ina mpango gani kukopesha Wajasiriamali vifungashio kama ambavyo benki zinavyokopesha fedha ili kuongeza ubora wa bidhaa?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi vijana wengi sana hasa waliomaliza vyuo wamejishikiza katika ajira ya ujasiriamali na wanahitaji vifungashio. Swali la kwanza; je, SIDO imefanya tathmini ya changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo na hasa hao vijana waliotoka vyuo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, SIDO haioni haja ya kuwa na utaratibu wa kushirikiana na taasisi za kifedha ili wanufaika wa mafunzo hasa vijana waweze kupata mitaji ya kuanzisha au kupanua shughuli zao za kiuchumi? Ahsante. (Makofi)
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana na kumshukuru Mheshimiwa Ntara kwa weledi na ushauri wake na huyu ni daktari msomi maana yake amesema kwamba vijana wajasiriamali wengi wana changamoto ya mtaji.
Mheshimiwa Spika, SIDO moja ya kazi zake ni kufanya au kuendeleza teknolojia mbalimbali za viwanda, lakini pia wanatoa mafunzo na uendelezaji wa biashara. Zaidi, wanafanya kutafuta masoko na uwekezaji na zaidi ni hii ambayo Mheshimiwa Mbunge amesema kuhusiana na mikopo ya kifedha kwa vijana na wajasiriamali wengine.
Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue ushauri wake kwamba SIDO sasa tuna nafasi ya ziada ya kufanya tathmini ya kina ili kuhakikisha tunaona changamoto zilizopo kwa vijana na hasa kwenye sehemu hii mahususi ya vifungashio. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, tayari Serikali kupitia SIDO inashirikiana na baadhi ya taasisi za kifedha kupitia mifumo hasa hivi viwanda ambao unasaidia, lakini mahususi unakwenda kwenye viwanda vikubwa au vya kati ambavyo wajasiriamali wengi hawana uwezo huo wa kukopa zaidi ya shilingi milioni tano na kuendelea. Kwa hiyo nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwamba tunachukua ushauri wake, lakini zaidi tutaendelea kuboresha kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda zaidi hapa nchini vya vifungashio, ambalo ndiyo tatizo kubwa katika nchi yetu kwa bidhaa ambazo ni nzuri zinazozalishwa. Kwa sababu bidhaa inaweza kuwa nzuri lakini ukifungasha kwenye kifungashio ambacho hakivutii au hakina ubora maana yake hata thamani ya bidhaa hiyo inakuwa ni ndogo. Ninakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved