Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 10 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 124 | 2025-04-23 |
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:-
Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Kijiji cha Igogo kwenda Igurubi Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora. Kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tanki moja (1) lenye ujazo wa lita 1,000,000, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 150 sanjari na ujenzi wa vituo 57 vya kuchotea maji.
Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 60% na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2025 na kunufaisha wananchi 71,726 waishio kwenye vijiji 18 vilivyopo katika Kata saba (7) za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’ila, Mwamakona, Igurubi pamoja na Kinungu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved