Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, katika mradi huo utajengwa na matenki kwa ajili ya kuhifadhia maji kwa sababu imekuwa ni changamoto kubwa sana kwani vijiji vingi vinakuwa vinajengewa miradi, lakini watu wanapata shida kwenda kuyafuata?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Mradi wa Maji wa Kijiji cha Mkalanga, Wilaya ya Kilolo lini utakamilika kwa sababu wananchi wamepata shida sana na wameusubiri kwa muda mrefu sana? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la kwanza la nyongeza. Kama nilivyojibu katika jibu la msingi, Serikali imekamilisha ujenzi wa tenki la lita 1,000,000. Pia, tunaendelea kulaza mabomba umbali wa kilometa 150. Tumeangalia pia vijiji vya Mwamharanga pamoja na Bukama vyenyewe viunganishiwe maji wakati mradi ukiwa unaendelea kutekelezwa kwani wenyewe una existing infrastructure ambazo wanaweza kuendelea kupata huduma ya maji bila kuwa na tatizo lolote.
Mheshimiwa Spika, swali la pili; upande wa Mkalanga, mradi huu unagharimu takribani shilingi milioni 391 ambapo mradi huu umefikia 95% na tunatarajia ufikapo mwezi Mei, mradi huu utakamilika. Nimuahidi Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati tutaenda nae mpaka Kilolo kuuzindua mradi huu ili wananchi wa eneo hilo waweze kupata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 2
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wakandarasi wengi nchini wameshindwa kuomba Miradi ya Maji mara baada tunapotangaza mfano wake uko katika Jimbo la Mbulu Mjini, tumetangaza visima viwili lakini hakuna mkandarasi aliyeomba kwa mara mbili na pengine nchi nzima; je, utaratibu ukoje sasa kwa pale ambapo Wizara imetangaza ama Serikali mara mbili, lakini hakuna aliyejitokeza? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kama nimelisikia vizuri swali lake. Tumekuwa na changamoto nchi nzima katika baadhi ya maeneo ambapo uchimbaji wa visima inategemea pia na aina ya vifaa mkandarasi anavyokuwanavyo. Kuna maeneo mengine kwa mfano Mkoa wa Singida tulipata changamoto katika Mradi wa Miji 28. Katika mradi huo wakandarasi wengi walikuja walijaribu kuchimba, lakini mashine zao zilishindwa kumudu hali halisi ya eneo husika na baadaye tukatangaza tena ili kupata ambae ataweza kuwa na vifaa kama hivyo.
Mheshimiwa Spika, kesi kama hiyo imeendelea kutokea katika maeneo mbalimbali, lakini Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba inafanya utafiti wa kina kuona namna gani wakandarasi watashauriwa wanapoomba kazi hizi waangalie namna ambayo itaendana na eneo husika ili waweze kutimiza mahitaji ya kandarasi hiyo. Ahsante sana.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 3
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itatekeleza miradi ya maji iliyoahidiwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu mwaka 2021 katika Vitongoji vya Nasaya na Masaninga? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ahadi za viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais pamoja na Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, sisi Wizara ya Maji tunachukua kwa uzito kabisa. Pale ambapo fedha zinapatikana, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge suala lake tutalifanyia kazi kwa uzito stahiki.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 4
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ziwa Victoria kwenda Mkoa wa Simiyu unasuasua sana. Ninataka kujua, ni lini mradi huu utakwisha ili wakazi wa Mkoa wa Simiyu wanufaike na maji? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza Mjika kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ziwa Victoria ni ndoto ya Wanasimiyu na ni ndoto ya Wabunge wote wa Mkoa wa Simiyu ambao wameendelea kuupambania sana. Mheshimiwa Rais aliridhia kutoa shilingi bilioni 440 kwa jili ya ujenzi wa mradi huu ambapo awamu ya kwanza tayari umeshaanza kutoka Nyashimo – Bariadi kwenda Itilima.
Mheshimiwa Spika, tumeshatangaza pia kandarasi ya pili kwa ajili ya mradi huu wa extension yake kupita Maswa mpaka Meatu. Nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, Mradi huu kwa Sekta ya Maji na Wizara ya Maji, sisi tunauchukulia kwa uzito kwa sababu una maslahi mapana kwa sababu unaenda kuhudumia wakazi takribani laki saba wanaokaa katika Mkoa wa Simiyu. (Makofi)
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 5
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, Serikali imechimba Mradi wa Maji wa Qaloda pale Dongobesh na Mradi wa Maji wa Getesh pale Tumati, imebaki tu kuleta fedha za mabomba ili kumaliziwa mradi ule. Je, lini mnaleta fedha za mabomba ili mradi ukamilike?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso alitoa maelekezo kwa Mameneja wetu wa Mikoa kuhakikisha kwamba tunapomaliza kuchimba visima cha kwanza ni kuhakikisha tunatengeneza point source wananchi waanze kupata huduma ya maji safi salama, lakini tukiwa tunatafuta fedha za kupanua mtandao ili wananchi walioko mbali na eneo la point source waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Spika, maelekezo ya Mheshimiwa Waziri tayari Katibu Mkuu ameshaanza kufanya mchakato wa kupeleka fedha ili bomba hizo ziweze kutandazwa na wananchi wa Mheshimiwa Flatei waweze kufurahia uwepo wa maji katika maeneo hayo.
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 6
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, ni lini Mradi wa Maji kutoka Milima ya Nongwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo utakamilika? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mradi huo ninafahamu kwamba uko katika hatua nzuri kabisa ya utekelezaji wake, lakini pia tunafahamu kwamba uko ndani ya mkataba kulingana na utekelezaji ambao tumeingia na mkandarasi. Kwa hiyo, ninaamini kabisa kwamba utakamilika ndani ya mkataba ambao tumesaini na mkandarasi. (Makofi)
Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila Mwamakona, Igurubi na Kinungu utakamilika?
Supplementary Question 7
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahadi za viongozi zimekuwa zikipewa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi na Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa ahadi toka mwaka 2017 ya kuchimba kisima kirefu katika Kata ya Kalulu, leo hii takribani miaka nane ahadi ile haijatekelezwa. Ninataka kufahamu; je, ni lini hasa kile kisima kitakwenda kuchimbwa na kutekeleza ahadi ya Waziri Mkuu? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana lakini pia ninashukuru sana swali la Mheshimiwa Hassan na kwa kazi nzuri sana anayoifanya kwa wananchi wake. Ninatambua kwamba ahadi hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya mwaka 2017 kwa upekee kabisa na kwa heshima na unyenyekevu ninaomba niipokee ili twende tukaifanyie kazi. Pia, nimwombe Mheshimiwa Mbunge tushirikiane ili tuone tunatatua kwa namna gani ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama yanayotokana na kisima hicho. (Makofi)