Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 10 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 127 | 2025-04-23 |
Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buyungu
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-
Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha zao la alizeti. Katika kuimarisha kilimo cha alizeti Wilayani Kakonko, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora, kuwapa vitendea kazi Maafisa Ugani ili waweze kuwafikia wakulima na kutoa ushauri wa kilimo bora cha alizeti.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mikakati hiyo, katika msimu wa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Halmashauri ya Kakonko imeanzisha mashamba manne ya mbegu katika Kata za Kiziguzigu na Rulenge. Pia, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetoa pikipiki 13 na kifaa cha kupima afya ya udongo (soil scanner) kwa Maafisa Ugani. Kifaa hicho kitawezesha kushauri wakulima matumizi sahihi ya mbolea.
Mheshimiwa Spika, baada ya kutekeleza mikakati hiyo na uzalishaji kuongezeka, Serikali itaendelea kuhamasisha wawekezaji kuanzisha viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved