Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kavejuru Eliadory Felix
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buhigwe
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 1
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imekiri kuwa Kakonko ni eneo zuri kwa kilimo cha alizeti na nchi yetu bado ina uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula. Je, Serikali ipo tayari kugawa bure mbegu bora za alizeti kwa wakulima katika Wilaya ya Kakonko? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; pamoja na umuhimu wa zao la alizeti bado wakulima hawana ufahamu wa kutosha. Je, Serikali imejipangaje kutoa elimu ya kilimo cha alizeti kwa wakulima hapa nchini? Ahsante sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli matarajio ya wananchi wengi ambayo Mheshimiwa Mbunge ameeleza ni pamoja na kutoa mbegu bure, lakini mkakati wa Serikali tulionao sasa hivi tumeweka ruzuku katika mbegu ili kupunguza gharama kwa wananchi kwa maana ya wakulima. Kwa hiyo, hatua ya sasa tumeongeza ruzuku, ninafikiri kadiri uwezo utakavyoongezeka wazo lake Serikali tutalifikiria kwa baadaye.
Mheshimiwa Spika, pia, kuhusu kuongeza elimu zao la alizeti katika Wilaya ya Kakonko jambo hilo tumelipokea. Tutawatuma Maafisa Ugani wetu waweze kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu, ili wananchi hao waweze kuingia katika kilimo cha alizeti. Ahsante. (Makofi)
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 2
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi. Je, ni upi mkakati wa Serikali kugawa mbegu za alizeti, ufuta pamoja na mpunga kwenye Kata ya Ivuna ambao walipata maafa na mazao yao yakaharibiwa ili kuwapooza? (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa hapo mwishoni ili kuwapooza?
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ili kuwatoa machungu ya kuharibikiwa na mazao yao?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimwondoe shaka tu Mbunge wa Jimbo la Momba Mheshimiwa Condester kwamba, moja ya mkakati wetu Serikali maeneo yakiwa na maafa yanapotokea, kama mafuriko na wananchi kuondokewa na mazao yao, mkakati ambao tumekuwa tukiufanya ni pamoja na kutoa mbegu. Kwa hiyo, tuandikieni hayo mahitaji nasi tutaleta mbegu bure kwa ajili ya kusaidia hao wananchi ambao wamepatwa na maafa hayo. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa kutekeleza falsafa ya BBT kwenye Majimbo ambayo hayana maeneo makubwa ya kilimo kama Vunjo? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba mkakati ambao tupo nao sasa hivi ni kuhakikisha kwamba, mradi wa BBT unakwenda katika majimbo yote nchini. Kwa hiyo, jambo hili lipo na tumesha-identify karibu maeneo mengine yote na tulishaziomba halmashauri kutuletea maeneo kulingana na ukubwa wake. Kwa hiyo, lipo katika utekelezaji na tunapotekeleza haina maana kwamba tutatekeleza katika maeneo makubwa kama ambavyo tunayo hapa Chinangali, Ndogoye na maeneo mengine. Kwa hiyo, hata katika maneeo ambayo ni madogo bado tutatekeleza mradi huo ikiwemo katika Jimbo la Vunjo. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 4
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa ambayo pia inalima alizeti, lakini kunakuwa na changamoto ya wakulima kupata mbegu bora na viuatilifu. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha wanapata mbegu bora na viuatilifu hasa Jimbo la Kalenga? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, mkakati tulionao sasa hivi moja, tunaongeza uzalishaji kwa kuingia makubaliano na wakulima, kwa maana ile tunaita contract farming ili waweze kuzalisha mbegu ya alizeti. Vilevile, tumeruhusu uagizaji wa mbegu bora za alizeti kutoka nje kuingia ndani ya nchi, lakini mbegu hizo zote zitaingia katika mpango wa ruzuku ambao tunaufanya katika mbegu za alizeti na mahindi. Kwa hiyo, niseme tu kwamba sisi tutaongeza hiyo kasi ili tuweze kuwafikia wananchi wa Mkoa wa Iringa na Jimbo la Kalenga. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Aysharose Ndogholi Mattembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 5
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. Kwa kuwa, Singida ni kinara wa kilimo cha alizeti nchini. Je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza pembejeo bora na kuwapatia mafunzo wakulima wake ili kuongeza tija katika kilimo hicho? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli katika zao la alizeti Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo Wizara ya Kilimo tunaitegemea, ndiyo mkoa ambao hata kazi kubwa ambayo tumekuwa tukiifanya ikiwemo kupeleka aina mbalimbali za mbegu za alizeti katika Mkoa huo kama vile OPV na zile mbegu za Hybrid, kwa hiyo, hayo yamekuwa yakifanyika.
Mheshimiwa Spika, ninamwondoa shaka Wizara tutaendelea kuleta mbegu bora katika Mkoa wa Singida na vilevile tutaendelea kutoa elimu kupitia Maafisa Ugani wetu ili kuhakikisha kwamba, alizeti inaendelea kuzalishwa kwa wingi ili tuweze kuondoa hii adha ya uhaba wa mafuta hapa nchini. Ahsante. (Makofi)
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Kakonko?
Supplementary Question 6
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, mwaka juzi, mwaka jana na mwaka huu wananchi wa Mkoa wa Rukwa wamepata mbegu za alizeti zisizofaa. Ni mkakati gani wa Serikali ambao wameufanya wa kufanya tafiti za kina kugundua mbegu hizo zisizofaa na zisirudi tena kwa wakati mwingine kuwatia hasara wananchi? Ninakushukuru sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba, mbegu kabla hatujaipeleka kwa wananchi huwa tunaichunguza kupitia taasisi yetu ya utafiti ya TARI na vilevile TOSCI kwa ajili ya kuithibitisha ubora wake na ASA wanalo jukumu la kusambaza mbegu hizo ambazo zimeshathibitishwa. Kwa hiyo, kama kuna makosa inawezekana yalitokea kutokana na mbegu ambazo wananchi walichukua katika maeneo mengine na ikaonekana sisi ndani tumesambaza.
Mheshimiwa Spika, jambo hilo tutalipitia na kuliangalia. Vilevile, tutachukua hatua thabiti kwa ajili ya kuhakikisha mbegu zisizofaa haziwafikii wakulima. Ahsante. (Makofi)