Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 10 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 129 2025-04-23

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wahitimu waliosoma katika Vyuo vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata usajili ili kuajiriwa nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, usajili wa wahitimu kutoka vyuo vya nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Vyuo vya Jumuiya ya Afrika Mashariki hufanywa na Mamlaka za Usajili au Bodi za Kitaaluma (Professional Bodies), kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Kabla ya usajili mhitimu hutakiwa kupeleka vyeti vya taaluma Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na wale wa stashahada na cheti hupeleka vyeti Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET), ili kufanya uthibitisho, ulinganifu wa sifa na kiwango cha elimu. Hivyo ninapenda kuwasihi wahitimu wote kutoka vyuo vya nje ya nchi kufuata utaratibu uliopo, ili kupata usajili. Ninakushukuru sana. (Makofi)