Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 152 2025-04-28

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -

Je, lini Serikali itasikiliza malalamiko ya watumishi dhidi ya Kikokotoo?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuwa sikivu muda wote kunapojitokeza hoja zinazohusu kikokotoo cha mafao kwa wastaafu. Katika kuonesha usikivu wake, kuanzia Julai, 2024 Serikali imeongeza malipo ya mkupuo kutoka 33% hadi 40% kwa wastaafu na kuanzia mwezi Januari, 2025 Serikali imefanya mabadiliko katika malipo ya pensheni kwa wastaafu kwa kupandisha kiwango cha chini cha pensheni kutoka shilingi 100,000 hadi 150,000 kwa Mifuko yote miwili, PSSSF na NSSF.

Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuonesha usikivu huo, Serikali imepandisha kiwango cha malipo ya pensheni kwa mwezi kwa wastani wa asilimia mbili kwa mwaka na kuwa Mifuko imeanza kulipa ongezeko hilo tangu mwezi Januari, 2025.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.