Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 13 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 154 | 2025-04-28 |
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeandaa mpango wa ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati kwa awamu. Katika mwaka 2024/2025, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya kwenye Kata ya Misughaa.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Isuna. Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Kimkakati zikiwemo Kata za Mang'onyi na Siuyu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved