Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martha Nehemia Gwau

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 1

MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri, nina swali moja la nyongeza. Je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha mkakati cha Misughaa ambacho Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo Miraji Mtaturu alishakiombea fedha? Ninashukuru.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE.ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 shilingi milioni 250 zitatolewa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya cha kimkakati kwenye Kata ya Misughaa.

Mheshimiwa Mbunge Mtaturu amekuwa akipaza sauti yake kuiomba Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan iweze kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki cha afya cha mkakati na Serikali sikivu, imemsikia na italeta fedha hizi kwa ajili ya kujenga kituo hiki cha afya ili kiweze kuwanufaisha watu wa Singida Mashariki.

Name

Livingstone Joseph Lusinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtera

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 2

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itatukumbuka Kituo cha Afya Kata ya Mvumi Mission kama ambavyo tumekuwa tukiomba siku zote?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE.ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha kwamba Kituo cha Afya cha kimkakati kinajengwa katika Kata aliyoitaja. Ninaomba nimtupe taarifa njema Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita italeta shilingi milioni 250 katika mwaka huu wa fedha, kwa ajili ya kuanza kujenga Kituo cha Afya cha kimkakati hicho ulichokitaja. (Makofi)

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 3

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, Kata za Jangalo, Lahoda na Mpendo ni Kata za mpakani na ziko mbali sana na huduma za afya. Ni upi mkakati wa Serikali wa kutoa fedha ili tuweze kujenga vituo vya afya kwenye Kata hizo, ahsante sana.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu mkubwa sana wa kuimarisha huduma za afya ya msingi na ndiyo maana katika kipindi cha miaka nine cha utawala na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, jumla ya shilingi trilioni 1.29 zimewekezwa katika kuimarisha Sekta ya Afya Msingi. Katika kipindi hicho cha miaka minne vituo vya afya 367 vimejengwa.

Mheshimiwa Spika, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Monni kwamba Serikali kwa kutambua umuhimu wa vituo vya afya alivyovitaja katika Jimbo lako kwa awamu itaendelea kuleta fedha kwa ajili ya kuvijenga vituo hivyo vya afya ili viweze kuwanufaisha wananchi wake.

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 4

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Ngongowele ni cha mwaka wa fedha 2021/2022, lakini kilipata shilingi milioni 250 tu mpaka leo kituo kile hakijapata pesa zingine na Kituo cha afya cha Mpengele hakina jengo la OPD.

SPIKA: Mheshimiwa, sasa hapo swali au unachangia, swali lako ni la nyongeza? Kituo kimoja cha afya unataka mchango, hebu uliza swali lako la nyongeza.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza ni kwamba, ni lini Kituo cha Afya cha Mpengele na Ngongowele vitapatiwa fedha ili viweze kukamilika?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta na kutoa fedha kwa ajili ya kuendelea kuimarisha huduma za afya msingi na imekuwa ikifanya hivyo kwa kuimarisha miundombinu katika sekta hii muhimu kabisa katika hospitali vituo vya afya na zahanati.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali italeta fedha katika vituo vya afya alivyovitaja kwa ajili ya kuvikamilisha ili viweze kutoa huduma za afya msingi nzuri kwa wananchi wake. (Makofi)

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 5

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri ya Itigi Jimbo ninaloliwakilisha, tuliahidiwa na Serikali kwamba tutaletewa pesa kwa ajili ya kujengewa kituo cha afya cha mkakati. Je, nasi tutapata katika awamu hii? Ahsante sana.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE.ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Massare amekuwa akifanya ufuatiliaji wa karibu kabisa ili kuhakikisha kwamba kituo cha afya cha kimkakati kinajengwa katika Jimbo lake. Ninaomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 kabla haujaisha, Serikali italeta shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ambacho amekuwa akikipazia sauti.

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU K.n.y. MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya kimkakati kwenye Kata za Isuna, Mang'onyi na Siuyu?

Supplementary Question 6

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha afya katika Kata ya Uyui ambayo iko kijijini katika Manispaa ya Tabora Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa njema Mheshimiwa Mwakasaka kwamba katika Mwaka huu wa Fedha 2024/2025 kabla haujaisha, Serikali italeta shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza kujenga kituo cha afya cha kimkakati katika Jimbo lako.