Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 155 2025-04-28

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-

Je, Serikali imechukua hatua gani kwa Vikundi hewa na udanganyifu kwenye mikopo ya asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikichukua hatua mara inapobaini uwepo wa vitendo vya udanganyifu na uwepo wa vikundi hewa wakati wa utoaji wa mikopo ya 10% kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutoa elimu kwa wanufaika zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa kutokana na udanganyifu ikiwa ni pamoja na kusitisha mikopo kwa vikundi vinavyohusika, kuanzisha uchunguzi, pamoja na kuwachukulia hatua watumishi wa umma walioshiriki au kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu za utumishi wa umma.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha utaratibu wa utoaji wa mikopo ya 10% unakuwa bora, Serikali imeanzisha mfumo wa kidigitali unaojulikana kama "Wezesha Portal” ambao unahakikisha vikundi vyote vinathibitishwa kwa njia ya kielektroniki kabla ya kupewa mkopo.