Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 156 2025-04-28

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kutenga Shule chache za Kata kuwa za bweni kwa kuwa, matokeo ya wanafunzi si mazuri?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa shule kuwa na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia, ikiwemo uwepo wa mabweni. Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024 – 2024/2025, Serikali imetumia shilingi bilioni 70.33 kujenga mabweni 537 katika shule za kata 270, ili zipandishwe hadhi kuwa kidato cha tano na sita. Kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni ujenzi wa shule mpya za kutwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi na watoto kutembea mwendo mrefu na kuongeza nafasi katika shule za kidato cha tano na sita.