Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 13 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 159 | 2025-04-28 |
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ukarabati wa Mahakama za Mwanzo West Meru na Nkoaranga, ambazo zimeachwa na kubakia magofu?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Tanzania imeendelea kutekeleza mpango wake wa ujenzi na ukarabati wa Majengo ya Mahakama wa mwaka wa fedha 2021/2022 – 2025/2026 kwa kuimarisha majengo katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyopo. Majengo haya yanajengwa na kukarabatiwa kwa awamu kwa kuzingatia Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Mahakama na kadri ya fedha zinavyopatikana.
Mheshimiwa Spika, ukarabati wa Mahakama ya Mwanzo Nkoaranga na Mahakama ya Mwanzo West Meru utafanyika kwa bajeti ya 2025/2026. Aidha, kutokana na mahitaji makubwa katika jimbo la Arumeru, mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imejenga jengo la kisasa la Mahakama ya Mwanzo Maji ya Chai, na lipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved