Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ukarabati wa Mahakama za Mwanzo West Meru na Nkoaranga, ambazo zimeachwa na kubakia magofu?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza. Kata za Ngalinanyuki, Uwiro, na Ngabobo ziko nyuma ya mlima Meru Kaskazini ambako ni mbali sana na mahakama ya mwanzo ya maji ya chai. Je, Serikali ina tamko gani kuhusu ukarabati wa Mahakama ya Mwanzo iliyoko Ngarenanyuki?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo tumefanya katika Mahakama ya Maji ya Chai pamoja na Oldonyosambu, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda kuhakikisha kwamba tunafanya ukarabati katika Mahakama hii ya Ngarenayuki kwa fedha ambayo tutapitisha kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2025/2026.
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ukarabati wa Mahakama za Mwanzo West Meru na Nkoaranga, ambazo zimeachwa na kubakia magofu?
Supplementary Question 2
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, Kata ya kikunde na Kata ya Pabi halikadhalika na Kata ya Tuhuli zina umbali takribani kilomita 80 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ambapo kuna Mahakama ya Mwanzo. Je, kuna mpango mkakati gani wa kuhakikisha kwamba kata hizi zinakuwa na Mahakama za Mwanzo?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema, Agosti 2022 Mahakama ilizindua mpango wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Mahakama. Mpango huo haujaacha kata yoyote, tarafa yoyote wilaya yoyote na mkoa wowote. Kata ya Kinguli na kata zingine kwa Mheshimiwa Omari nao umezingatiwa katika mpango na tutafanya ukarabati.
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ukarabati wa Mahakama za Mwanzo West Meru na Nkoaranga, ambazo zimeachwa na kubakia magofu?
Supplementary Question 3
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninataka kufahamu, je, wamefikia hatua ipi katika ujenzi wa Mahakama katika Wilaya ya Ileje?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Mahakama katika Wilaya ya Ileje unaendelea na tunategemea kwamba utakamilika mwaka ujao wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved