Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 13 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 161 | 2025-04-28 |
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo la upungufu wa Maji katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa Mkoa wa Kigoma ni wastani wa 72.8% vijijini na 79.8% mijini. Serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025 imekamilisha utekelezaji wa miradi 17 katika Wilaya za Buhigwe, Kigoma, Kibondo, Kasulu, Kakonko pamoja na Uvinza mkoani Kigoma. Aidha, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 47 ya usambazaji maji pamoja na uchimbaji wa visima 30 katika wilaya hizo ambapo ujenzi wa miundombinu rahisi ya kutolea huduma (point source) 13 umekamilika na zinatoa huduma wakati 14 zinaendelea na ujenzi kwa kila jimbo kupitia Programu Maalum ya Uchimbaji wa Visima 900.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali itatoa kipaumbele cha kukamilisha miradi inayoendelea sambamba na kufanya upembuzi yakinifu wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kwa lengo la kunufaisha Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi. Lengo ni kuhakikisha kwamba wananchi wa Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved