Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo la upungufu wa Maji katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji Mkoani Kigoma kwa kutumia chanzo cha Mto Malagalasi?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; katika Halmashauri ya Kibondo, Kata ya Mabamba, Shule ya Sekondari Kumgogo maji hutoka mara moja moja na hivyo wanafunzi wanapata shida ya maji. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji katika shule hiyo ya Sekondari?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ninapenda pia kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha kwamba anawapigania akinamama wa Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kwamba zao la maji na ndiyo suluhisho la kudumu kwa maji kutoka mara moja moja. Kama ambavyo amesema katika ile shule inayopatikana Kibondo ni kwamba Serikali imeendelea kuongeza program nyingi. Program ya kwanza ni ya visima 900 lakini program ya pili ni mradi wa miji 28 ambapo unagharimu bilioni 35 ambao uko katika 45% ya utekelezaji ambao tunatumia Mto Ruchugi lakini vile vile tuna mradi ambao RUWASA wanaendelea nao, ambao miradi takribani miradi 37 yenye gharama ya bilioni 13.5

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Mradi wa Maji Mto Malagarasi awali tulifanya usanifu ili uweze kuhudumia maeneo ya Kaliua pamoja na Urambo lakini baadaye Ziwa Victoria likaleta kwa sababu ndicho chanzo cha uhakika.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu tunakwenda kutumia mradi wa Ziwa Tanganyika kama ambavyo nimejibu katika jibu la msingi tayari Serikali imeanza kutafuta mtaalam mshauri ili afanye upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina ili aweze sasa kuona namna gani tutatumia maji ya Ziwa Tanganyika kwa Mikoa ya Kigoma, Rukwa pamoja na Katavi. Kwa hiyo tunaamini kwamba maji hayo yataweza kuwa suluhisho la kudumu kwa wananchi wa Mikoa ya Kigoma Rukwa pamoja na Katavi. Ahsante sana.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo la upungufu wa Maji katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Ninataka kujua mkakati wa Serikali wa kumaliza tatizo la maji katika Kijiji cha Hunyali?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na pia nimshukuru Mheshimiwa Gerete kwa swali lake. Mradi huo wenye gharama ya milioni 830 tayari mwezi Februari Mheshimiwa Waziri wa Maji alielekeza milioni 141 ifike pale kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa mradi huo. Hivyo mradi huo unaendelea kutekelezwa. Ahsante sana.

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo la upungufu wa Maji katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma?

Supplementary Question 3

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kutosha ili kumalizia Mradi wa Maji wa Munyo katika Jimbo la Ikungi Magharibi? Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba inatekeleza miradi yake yote nchini kulingana na upatikanaji wa fedha. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwa upande wa Singida tuna miradi mingi inaendelea. Mradi huu ni kipaumbele kwetu na fedha tayari tumeshawasilisha hati za madai Wizara ya Fedha kwa ajili ya mkandarasi kulipwa ili mkandarasi aweze kukimbiza kazi na ikamilike kwa wakati. Ahsante sana.

Name

Josephine Tabitha Chagulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo la upungufu wa Maji katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma?

Supplementary Question 4

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Chato?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya maji katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita, lakini vilevile Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa Mradi wa Miji 28 katika Mji wa Chato. Huu mradi utakapokamilika Wanachato watakuwa wameondokana kabisa na tatizo la maji. Ahsante sana.