Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 164 2025-04-28

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:-

Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kata ya Kipugila, inapata huduma ya mawasiliano kupitia minara iliyojengwa katika Vijiji vya Kipo kwa mnara wa Halotel na Kipugila mnara wa TTCL.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ameuliza swali kuhusu jitihada za Serikali katika kutatua changamoto ya mawasiliano katika kata hii, inaashiria kuwa bado kuna changamoto. Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafanya tathmini kwenye kata hii ili kubaini mahitaji halisi ya mawasiliano na endapo ikibainika kuwepo kwa tatizo la mawasiliano katika kata husika, itaingizwa katika zabuni ya miradi itakayotekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.