Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwantumu Mzamili Zodo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 1
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Kipugila ambayo Mheshimiwa Hawa ameuliza swali kuna mnara mmoja wa halotel, lakini bado kuna mawasiliano ya kusuasua. Swali la kwanza; je, ni lini sasa Serikali itajenga minara mingine kama mnara wa Halotel, Voda na Mixx By Yas ili kuhakikisha wananchi hao wanapata mawasiliano ya uhakika?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; katika maeneo ya Jimbo la Tanga Mjini, yaani maeneo ya Mwang’ombe na Kange palepale mjini pia bado kuna mawasiliano ya kusuasua na minara ipo. Je, ni nini changamoto hasa katika maeneo hayo? Ahsante.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza, katika eneo hili la Kipugila kuna mnara wa Halotel lakini mawasiliano hayajakaa vizuri. Ninaomba tu nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kama mnara upo basi kwa niaba ya Waziri nitoe maagizo kwa watoa huduma wa Halotel kuhakikisha wanakwenda kuboresha kwa ku-upgrade mnara huu, kuhakikisha teknolojia zote zinaweza kuwekwa. Kama 2G ndiyo inayofanya kazi basi 3G na 4G pia wakazi-upgrade.
Mheshimiwa Spika, kwa watoa huduma wengine nje ya Halotel (Voda, Yas na TTCL) nao kuweza kupatikana kama namna alivyowataja. Basi kuna matumizi ya pamoja ya miundombinu ili kuokoa muda, wanaweza kuwasiliana na watu wa Halotel wakatumia mnara huu kwa pamoja kama co-location. Pia, wanaweza wakafanya roaming ili wananchi waweze kupata huduma ya haraka na yenye uhakika.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusiana na Tanga pale Maweni, maeneo haya yana mawasiliano ya shida. Niweze tu kumwomba Mheshimiwa Zodo, tuwasiliane tupate location sahihi kabisa za hili eneo ili tuweze kuwaagiza wataalam wetu waweze kufuatilia kwa nini eneo lile lina minara, lakini bado hakuna mawasiliano.
Mheshimiwa Spika, sasa wakati mwingine huenda kwa sababu kuna blockage tu kama maghorofa marefu ama miti ama ni jiografia (miinuko na mabonde), lakini kama hivi vyote havipo basi tukiipata location hizi coordinates zitatusaidia kuona tatizo ni nini ili tuje tutatue. (Makofi)
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu ya TTCL katika Vijiji vya Marendego, Makolo na Kandawale?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fransis Ndulane, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, minara hii ya TTCL katika vijiji hivi ulivyovitaja Mheshimiwa Mbunge nitavisimamia kwa kuhakikisha wataalam wanakwenda kuona hawa wakandarasi wanajenga huu mnara ndani ya wakati wa mkataba. Ahsante.
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 3
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kunipa nafasi nami niulize swali la nyongeza. Katika Jimbo la Moshi Vijijini Kata ya Okaoni, Uru Shimbwe, Old Moshi Mashariki na kwingine kuna shida kubwa ya mawasiliano. Ni lini Serikali itapeleka minara ili wananchi hawa waweze kufaidika na mawasiliano? Ahsante sana.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Felista Njau, dhamira ya Serikali kote alikokutaja ni kuhakikisha vijiji, vitongoji na maeneo yote yanapata mawasiliano ya uhakika.
Mheshimiwa Spika, hivyo, tunaendelea na ujenzi wa minara mbalimbali, kama unavyofahamu minara ya 758 utekelezaji unaendelea na tunatarajia Mei kukamilika na tuna minara 632 na bado tuna batch nyingine za minara mbalimbali ya TTCL tutakuja kuyafikia maeneo yote haya.
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 4
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, Kata ya Lukumbule katika Kijiji cha Kazamoyo na Imani kilichopo mpakani mwa Mto Ruvuma kina tabu sana ya mtandao. Ni lini Serikali itajenga mtandao katika maeneo hayo?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mpakate, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, maeneo yote ya mpakani tunaendelea kuyafanyia kazi na nimeshafanya ziara baadhi ya mipaka ili kuhakikisha maeneo yote ya mipakani sasa kupitia changamoto tunazokutana nazo katika ziara yanaweza kufanyiwa kazi. Hivyo, nimtoe hofu hata hii kata aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tuwasiliane kwa karibu ili niweze kufuatilia kwa ukaribu na kuhakikisha mawasiliano yanaweza kufikishwa.
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 5
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Monduli ina changamoto kubwa ya mawasiliano hususan kwenye Kata za Engaruka, Selela na Esilalei. Je, ni upi mkakati wa Serikali sasa kutatua changamoto hii?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum, kwamba maeneo ya Monduli kuna maeneo kwenye hii kata aliyoitaja mawasiliano hayaridhishi, ninaomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira. Sisi kama Serikali tutaendelea kuhakikisha tunayafikia maeneo yote haya na kata hii aliyoitaja nitakufikia hapo ili tuweze kuwasiliana kwa karibu.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. MWANTUMU M. ZODO K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kata ya Kipugila Rufiji?
Supplementary Question 6
MHE. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, kwenye Kata za Kilema, Marangu Magharibi na Mwika Kaskazini kule Vunjo kuna shida sana ya mawasiliano na mawasiliano yaliyopo ni hafifu yanaingiliwa sana mawasiliano ya nchi jirani. Je, ni lini mtagawa hiyo minara 638 kwa awamu ya pili ili tuweze kupewa minara ya kutosha?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, maeneo haya yote aliyoyataja yapo katika mikakati ya Serikali. Kadri tunavyopata fedha nimhakikishie tutayafikia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya ndani ya nchi na si minara ya nchi jirani.