Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 165 2025-04-28

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:-

Je, nini kauli ya Serikali juu ya Wanawake wanaotupa watoto?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inakemea na kulaani kitendo cha baadhi ya wanawake kutupa watoto kwa lengo la kukwepa jukumu lao la msingi la kusimamia malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto. Hivyo, ninapenda jamii itambue kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wanawake watakaokutwa na hatia ya kutenda kosa hilo na kuadhibiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto, Sura ya 13, Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 pamoja na sheria nyingine za nchi zilizotungwa kwa suala hilo.

Mheshimiwa Spika, ninawasihi wanawake na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kutupa watoto. Aidha, endapo itatokea kuna mtu ameshindwa kutekeleza jukumu la malezi ya mtoto basi atoe taarifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Ofisi za Ustawi wa Jamii ambapo watawajibika kuweka mpango wa huduma mbadala kwa mtoto husika sawa na matakwa ya kifungu Na. 94(5) cha Sheria ya Mtoto Sura ya 13. Ahsante.