Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya Wanawake wanaotupa watoto?

Supplementary Question 1

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza, pamoja na majibu mazuri ya Serikali. Swali la kwanza; je, ina takwimu halisi ya mambo haya, kwa sababu inaonekana yamekuwa yakiongezeka kila siku?

Mheshimiwa Spika swali la pili; kwa sababu ya nyongeza hiyo ambayo kila siku imekuwa ikipigiwa kelele, Serikali haioni sasa ipo haja ya kuboiresha sheria hii ili ziwe kali zaidi? Ninakushukuru sana.

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninapenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeleta mafanikio makubwa kupitia mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika hatua ambazo zimechukuliwa. Kuna madawati 1,103 lakini kuna Mahakama 131 za Watoto ambazo zimefunguliwa na kumeanzishwa vituo 3,963 vya kulelea Watoto; pia, tuna vituo vya kulelea watoto mchana 2,649. Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba tunawatunza watoto, kuwalea na kuwapa stahiki zao zote jinsi zinavyohitajika.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Serikali inaendelea kuchukua sheria kali; sheria ambazo nimezieleza katika jibu langu la msingi; Sheria ya Mtoto, Sura Namba 13, ni adhabu kali ya faini isiyozidi shilingi milioni tano. Pia, kuna kifungo cha miezi sita na mengineyo ambayo jinsi matokeo ya udhalilishaji yanavyotokea basi adhabu hizo zinaweza zikatolewa kwa pamoja.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Je, nini kauli ya Serikali juu ya Wanawake wanaotupa watoto?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Wanawake hawa wanaowatupa watoto hawawatupi kwa sababu wanapenda. Kunakuwa kuna visababishi vingi vinavyosababisha wafikie hatua hiyo. Kwanza, kuanzia utungwaji wa mimba...

SPIKA: Mheshimiwa Paresso, uliza swali.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, sijui ninaulizaje. Je, Serikali haifikirii kwamba iko haja ya kuanzisha vituo vya utoaji wa nasaha kwa wanawake hawa kuliko tu kutumia sheria?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ina madawati 420 katika vituo vya polisi na katika jamii zetu nchini. Tunawaomba wananchi wanapofikwa na tatizo hilo basi moja kwa moja waende katika ofisi ya ustawi wa jamii wamwone afisa ustawi ili kumwelekeza na kumpa taratibu zote za malezi na makuzi kwa ajili ya Watoto.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawapenda sana na inawajali watoto na ndiyo maana ameweka vitu vingi kwa ajili ya watoto ili waendelee hadi wanapofika umri wa miaka 18 kuweza kujitegeme. Ahsante sana.