Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 166 2025-04-28

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA HASSAN TOUFIQ aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha upimaji wa ardhi unafanyika katika Vijiji vyote Tanzania Bara?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika ardhi za vijiji, jumla ya vijiji 10,987 kati ya vijiji 12,333 vilivyosajiliwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI vimepimwa mipaka yake. Vijiji vilivyoandaliwa Mipango ya matumizi bora ya ardhi ni 4,346 sawa na 35.24% ya vijiji 12,333. Uandaaji wa mipango hiyo umewezesha kutambua vipande vya ardhi 259,080 na kutolewa hatimiliki za kimila.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutenga fedha kupitia bajeti ya Serikali ambapo kila mwaka Serikali hutenga fedha kwa ajili ya kazi hiyo. Ni matarajio ya Serikali kukamilisha zoezi hili kutegemea upatikanaji wa fedha.