Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA HASSAN TOUFIQ aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha upimaji wa ardhi unafanyika katika Vijiji vyote Tanzania Bara?
Supplementary Question 1
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili. Swali la kwanza; nini kauli ya Serikali kwa vijiji vilivyosajiliwa, lakini bado kuna migogoro ya mipaka?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali ina mkakati gani wa kuharakisha mipango ya matumizi bora ya ardhi ili walau ifikie 60%? (Makofi)
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum na nitayajibu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, moja, anataka kujua kauli ya Serikali kwa vijiji vilivyosajiliwa, lakini bado kuna migogoro ya ardhi. Kimsingi tumeendelea na juhudi mbalimbali za kutatua migogoro ya ardhi hapa nchini, juhudi ambazo kimsingi ninadhani Waheshimiwa Wabunge wanakiri kwamba sasa tunakwenda kwa mwendo ambao ni mzuri zaidi. Kauli ya Serikali ni kuendelea kutatua migogoro hii ambayo kimsingi wakati mwingine haianzishwi na ile mipaka ila ni utashi tu wa kibinadamu ambao wananchi wanaweza wakawa wametofautiana katika uelewa wao.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili; mkakati wa Serikali katika kupandisha viwango vya kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kutoka hiyo 35% angalau ifike 60%. Kwa kweli tunaishukuru sana Serikali ya Mama Samia na hapa ninapoongea hivi karibuni tumepewa karibu shilingi bilioni tano ziko kazini, vijana wako kazini wanaendelea kupitia vijiji mbalimbali kuviwekea mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Mheshimiwa Spika, ni matarajio yetu kwamba, upatikanaji wa fedha kadri utakavyowezeshwa na Serikali, Wizara itaendelea kuweka mipango mizuri ya matumizi katika maeneo ya vijiji vyetu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved