Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 167 2025-04-29

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Tauhida Cassian Gallos, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha kuwa wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wanaendelea kunufaika na Mfumo wa Hifadhi ya Jamii hapa nchini, Serikali imeweka utaratibu wa kuwawezesha wazee waliokuwa katika Sekta Binafsi kuendeleza uanachama wao katika Mfuko wa NSSF hadi kufikia miaka 70. Ahsante.