Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Supplementary Question 1

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je; kuna maslahi yapi ya ziada ambayo Serikali inayatoa mahususi kwa ajili ya wazee?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kinga zipi za wazee zinazolindwa kisheria na Serikali? (Makofi)

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Tauhida. Kwanza; nimshukuru na kumpongeza kama jinsi wanavyofanya Waheshimiwa Wabunge wengine, lakini yeye amekuwa mahiri sana katika kutetea haki za wazee na makundi maalum hasa yakiwemo wanawake na watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali lake ni kwamba kwa upande wa Serikali, maslahi yanayotolewa kwa wazee mojawapo ni pamoja na kuangalia ustawi wao katika masuala ya afya na ya kiuchumi. Katika Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kusimamia vizuri sana mpango uliopo wa kuendeleza kaya maskini au duni kwa Mpango wa TASAF kupitia Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa pia na mpango wa matibabu bure ambao ni maslahi ambayo wazee wamekuwa wakinufaika nayo ikiwa ni pamoja na kutambua changamoto za wazee na kuweza kuwasaidia kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba, kuna mpango wa msamaha. Kwa mfano, maslahi ya kikodi ya ardhi, wazee wanasamehewa kulingana na umri ambao umekuwa justified kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna huduma za upendeleo ambayo ni maslahi wazee wamekuwa wakiyapata, mojawapo ikiwa ni kutoa upendeleo kwenye maeneo ya misongamano labda pale kunapohitaji huduma ya jamii kama vile kwenye kupiga kura, zoezi kubwa ambalo litampa ushindi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan; wazee watatangulia mbele kupiga kura. Pia, huko hospitali kwenye matibabu ni moja ya maslahi ambayo wazee wanapewa kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali lake la pili la kuhusiana na kinga za kisheria ambazo wazee wanazo. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Katiba yake ya Mwaka 1977 inatoa haki kwa wazee. Katika Ibara ya 11(1) inaeleza kuhusiana na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii hasa kwa kundi la wazee, lakini pia na wakati wa maradhi au watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Tanzania imekuwa nchi ya pili na ni jambo la kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa na Sera mahususi ya Wazee ya Mwaka 2003 na sasa tupo kwenye mchakato kupitia Wizara husika ya kwenda kupata Sheria ya Wazee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria hii imeweka maainisho ya kuzitaka Mamlaka za Serikali; Serikali Kuu, Serikali za Mitaa pia upande wa familia na mawakala wa hiyari kuhakikisha kwamba wanaangalia kwanza kuwatambua wazee na kuhakikisha kuna matunzo kwenye masuala ya umaskini, huduma za afya, ushirikishwaji pamoja na uundaji wa mabaraza ya wazee, ili kuweza kuhakikisha kwamba wanahudumiwa.

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Supplementary Question 2

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali lakini hapa wazee aliowazungumza ni wale waliopo kwenye Sekta Binafsi. Wapo wazee ambao wamekuwa na mchango mkubwa wa uzalishaji katika Taifa letu, lakini wapo katika sekta isiyo rasmi. Serikali haioni sasa kwamba, kuna umuhimu wa kuja na mpango madhubuti unaoeleweka tofauti na hii mipango ambayo mingi inaonekana ipo katika huruma zaidi na siyo katika sheria?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shangazi, Serikali imeweka mpango siyo tu kwa wazee walio katika Sekta Binafsi, wameangaliwa pia wazee wastaafu ambao walikuwa kwenye utumishi wa umma. Pia, wameangaliwa wazee ambao wapo katika sekta zisizo rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufanya hivyo kupitia Mfuko wa NSSF kupitia hili Bunge lako Tukufu tulibadilisha sheria hapa na tukaweka utaratibu wa kwamba, mafao sasa na masuala ya uchangiaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, hata mtu yeyote ambaye alikuwa kwenye Sekta Binafsi, Utumishi wa Umma au alikuwa nje ya mfumo wowote ule, ana uhiyari wa kuweza kuchangia kwenye huu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, ili aweze kupata masurufu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, ile Sera ya Wazee inajumuisha wazee wote bila kubagua ikiwa ni pamoja na kama nilivyosema awali, takwa la Ibara ya 11(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, haya maslahi ni ya wazee wote nchini kwa kuangalia kulingana na hali na tuna jukumu kubwa la kuwatambua kwa hali zao na sifa zao za kiuchumi na hali walizonazo, ili waweze kuhudumiwa na Serikali.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Supplementary Question 3

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri kama swali la msingi linavyosema kuna wazee zaidi ya 60%, tunafahamu kilimo ndicho kinatumika katika Taifa letu. Hawa wazee ambao wamelisaidia Taifa hili kwa kilimo na leo hii wamekuwa wazee wananufaikaje na NSSF, ili waweze na wao kuendeleza maisha yao? Hatuoni kuna haja ya kubadilisha hizi kanuni na kuwaona kundi kubwa hili la wazee ambao wapo vijijini wanahitaji kupata mafao ya aina hii? (Makofi)

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye majibu ya swali la msingi na kwenye hatua ya pili ni kwamba hata hao wazee walio kwenye kilimo, ambao ndio tunasema sekta isiyo rasmi, ni rasmi kwa maana ya kutambulika kwa sababu ina Wizara yake mahususi, tunawatambua. Hata NSSF kwa sasa mtu yeyote ili mradi tu amekidhi masharti na vigezo ambavyo vipo hasa kwa kuangalia umri na utu uzima, anaruhusiwa kupeleka michango yake NSSF kwa kiwango ambacho itakuwa ni kulingana na uwezo wake wa kiuchumi. Kwa hiyo, tunawaangalia kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata pia kwenye huduma nyingine za kiupendeleo zote hizi zinawagusa wazee katika sekta zote. Tulichobakiza ni hiyo hatua ya kwenda kutunga sheria, ili mambo haya yaweze kusimamiwa na kutekelezwa kwa kadri ambavyo sera inataka. Pili, kuweka ule umuhimu na msisitizo wa mamlaka za Serikali kuu na Serikali za Mitaa kuendelea kusimamia vizuri na kuratibu utoaji wa huduma za wazee.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Tanzania Visiwani, wazee wanapata posho kutokana na sera ya kule. Je, hatuoni kwamba kuna umuhimu sasa na Tanzania Bara kukawa na sera ya kuwapatia posho wazee? (Makofi)

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali la Mheshimiwa Mnzava, ni kweli kwa upande wa Tanzania Visiwani wameanza utaratibu huo na sisi kwa sera yetu hii ambayo ni ya mwaka 2003, moja ya maeneo ambayo yamewekewa mkazo ni pamoja na hili la kuangalia hali za kiuchumi na kuwanusuru wazee katika lindi la umaskini na changamoto za kiuchumi. Kwa hivyo, nimelipokea na tutaendelea kulifanyia kazi kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara husika, ili kuweza kuona hali ya kiuchuni kama itaruhusu basi hiyo itatekelezwa. Ahsante.

Name

Kasalali Emmanuel Mageni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuhakikisha Wazee kuanzia umri wa miaka 60 nchini wanaingia katika Mfumo wa Hifadhi ya Jamii?

Supplementary Question 5

MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Suala la manyanyaso na usumbufu kwa wazee wastaafu kwenye nchi hii limekuwa ni utamaduni wa kawaida wanavyokuwa wanafuatilia mafao na stahiki zao. Je, Serikali haioni kwamba upo umuhimu wa kutunga sheria kali inayotoa adhabu moja kwa moja kwa mtumishi au afisa yeyote wa Mamlaka ya Hifadhi ya Jamiii anayenyanyasa na kuchelewesha mafao ya mzee? Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nitambue kweli masuala ya unyanyasaji kwa kipindi cha nyuma yalikuwepo kwa sababu kumnyima mtu haki yake au kutokumlipa mtu ujira wake kabla jasho halijakauka ni sawa na kumnyanyasa au kumwonea na kuvunja haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kupitia Bunge lako Tukufu tulishafanya marekebisho hapa ya Sheria ya NSSF na PSSSF ambazo zinamtaka mwajiri kwanza kuwasilisha michango ya mfanyakazi kwa wakati. Hatua ya pili, ndani ya siku 30 baada ya kustaafu anapaswa kuwa amelipwa mafao yake. Hilo jambo linasimamiwa kisheria na uzoefu uliopo sasa kwa sababu ya teknolojia kubwa na mapinduzi ya TEHAMA kupitia Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alielekeza na tumetenga fedha. Tayari tumeshaanza kuwalipa hata kabla ya siku saba, mtu anapata mafao yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo la namna ambayo nimeeleza kwamba sheria kuchukua hatua kali. Sheria hii inataka pia Mfuko wenyewe wa NSSF ama PSSSF, ikitokea mwajiri hakuwasilisha michango, anaweza kupelekwa Mahakamani by summary suit, akaenda kushtakiwa na kuchukuliwa hatua kali ili kuweza kulinda haki na stahiki za hawa wafayakazi wastaafu.