Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 168 2025-04-29

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha Mradi wa Stendi ya Ngangamfumuni - Moshi Mjini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Ngangamfumuni katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ulianza kutekelezwa mwaka 2019 kwa Mkataba wa shilingi bilioni 28.9 ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 7.5 zimetolewa na mradi umefikia 51% ya utekelezaji. Aidha, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga bajeti ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa mradi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa stendi hii, kadri hati za malipo zitakavyokuwa zikiwasilishwa hadi mradi utakapokamilika. Ahsante.