Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha Mradi wa Stendi ya Ngangamfumuni - Moshi Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana na ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa kukwama kwa mradi huu kwa miaka mitatu nyuma siyo tatizo tena la fedha kwa sababu Wizara ilishakubali, tatizo kubwa ni Mkadarasi CRJE ambaye amekuwa na masharti magumu na ahadi za uongo kurudi site na kwa kuwa, tulienda mpaka Ofisi za TAMISEMI tukiwa na Mkurugenzi, Mstahiki Meya na Mwakilishi wa RAS tukafanya naye kikao na hajarudi; je, Serikali ipo tayari kutumia mbinu mbadala ili kumshinikiza arudi site?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa sababu kile ni chanzo cha mapato na muda ambao umepita umeshakuwa mkubwa na fedha zikiwa zimeshatumika kiasi, Serikali ipo tayari sasa kuvunja mkataba kama atakataa sasa kurudi tena site? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba Mkandarasi wa Ujenzi wa Stendi ya Ngangamfumuni aliacha site kwa kipindi cha takribani miaka miwili au mitatu kama Mheshimiwa Mbunge Tarimo alivyosema na kulikuwa na changamoto ya management ya mkataba kati ya Mkandarasi na Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na sababu hizo, tumekubaliana na tumefanya vikao. Tulifanya kikao tarehe 01 Januari, 2025 na mwezi Februari tulifanya vikao pia kati ya Ofisi ya Rais - TAMIESMI, Wizara ya Fedha, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kukubaliana na Mkandarasi arejee kwenye site aendelee kufanya kazi. Hivi sasa tupo hatua za mwisho za makubaliano kati ya Serikali na Mkandarasi ili kuhakikisha kwamba anarejea site na kuendelea na ujenzi wa stendi ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea na negotiations hizo kuhakikisha kwamba mkandarasi anarejea. Kama itatokea hajakubaliana na mazungumzo yetu kati yetu na Serikali, basi Serikali itachukua hatua nyingine ikiwemo kuvunja mkataba kwa mujibu wa sheria na taratibu, ili tuhakikishe tunakwamua mkwamo wa Ujenzi wa Stendi ya Ngangamfumuni. (Makofi)
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha Mradi wa Stendi ya Ngangamfumuni - Moshi Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Chemba ni Mji ambao unakua kwa kasi sana, lakini hauna stendi ya kisasa. Ninataka kujua, upi mpango wa Serikali wa kujenga stendi ya kisasa kwenye Mji wa Chemba? Ahsante sana.
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ni moja ya halmashauri ambazo tayari tulishatoa maelekezo Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuandaa andiko la kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa. Pia, tulielekeza kutafuta eneo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Monni kwamba, Serikali inatambua umuhimu na uhitaji wa stendi ya kisasa katika Halmashauri ya Chemba na tayari tulishatoa maelekezo kwa Halmashauri. Kinachofuata ni kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo kwa awamu. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha Mradi wa Stendi ya Ngangamfumuni - Moshi Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Halmashauri ya Kibondo imeshaandika Andiko la Mpango wa Kujenga Stendi ya Kisasa katika Jimbo la Muhambwe. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha wananchi wa Muhambwe wanapata stendi ya kisasa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninawapongeza Halmashauri ya Kibondo kwa kuandika andiko la ombi la ujenzi wa stendi ya kisasa pia ninawahakikishia tu kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha tunaendelea kuangalia uwezekano wa kupata fedha, kwa ajili ujenzi wa stendi za kimkakati katika Halmashauri zenye uhitaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo ni maelekezo ya Serikali kwamba halmashauri pia kupitia mapato yao ya ndani wahakikishie wanatenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi hizi, kwa sababu stendi hizi ni mahitaji ya wananchi katika maeneo hayo na Halmashauri pia zinaendelea kukusanya fedha za ndani kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali. Kwa hiyo, pamoja na Serikali Kuu na uandishi wa miradi ya kimkakati, lakini pia ni wajibu wa Halmashauri kuendelea kutenga fedha. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tumelipokea andiko hilo na tutatafuta fedha pia tutashirikiana na Halmashauri kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa awamu. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved