Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 169 2025-04-29

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi ya Kisasa – Makete kupitia miradi ya kimkakati ya Serikali?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kujenga na kuboresha stendi za mabasi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Makete inayo stendi yenye eneo la ukubwa ekari 3.1 katika eneo la Mabehewani. Stendi hii iliboreshwa na Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri, ambapo kiasi cha shilingi milioni 40 kilitumika na stendi hii inatumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri ya Makete imetenga shilingi milioni 100 ili kuboresha miundombinu ya Stendi ya Mabehewani. Aidha, ili kuwa na stendi kubwa ya kisasa zaidi, Halmashauri ya Makete imetenga eneo la ekari 24.5 na sehemu ya eneo hilo itatengwa kwa ajili ua ujenzi wa stendi ya kisasa. Ahsante. (Makofi)