Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 170 2025-04-29

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:-

Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejenga shule mpya ya Sekondari Mbale ambayo imesaidia kupunguza idadi ya wanafunzi katika shule ya Bukene kutoka 589 (wavulana 262 na wasichana 327) hadi 488, (wavulana 203 na wasichana 285), hivyo kupunguza tatizo la ikama ya walimu katika shule hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari Bukene ina uhitaji wa Mwalimu mmoja wa Fizikia, waliopo ni watatu. Hisabati uhitaji ni mwalimu mmoja, waliopo ni watatu. Hivyo, shule hii haina upungufu wa walimu wa masomo ya fizikia na hisabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuendana na ongezeko la shule na idadi ya wanafunzi, Serikali itaendelea kuajiri walimu kadri ya upatikanaji wa fedha.