Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?
Supplementary Question 1
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipata fursa ya kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali kadhaa ya sekondari ndani ya Jimbo la Bukene. Karibu sekondari zote kwenye changamoto zao walitaja upungufu wa Walimu wa Fizikia na Hesabu kama ni changamoto kubwa sana. Nililichukua tatizo hilo na kuliwasilisha Serikalini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, ninaipongeza Wizara kwamba, kwa kipindi hiki kifupi cha tangu mwezi Oktoba, 2024 ninayo taarifa kwamba mwezi Machi, mwezi uliopita tumepata mgao wa walimu kupitia ajira mpya, walimu kama 74 wa masomo ya fizikia na hesabu na hivyo kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa fizikia na hesabu. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kupokea pongezi kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Bukene kwa kumaliza tatizo la Walimu wa Fizikia na Hesabu kwa kipindi kifupi tu cha tangu mwezi Oktoba walipoleta changamoto hiyo, mpaka leo hii mgao wa mwezi uliopita umemaliza tatizo hilo? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapokea pongezi hizo, ni dhahiri Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada zote kuhakikisha inaendelea kuimarisha Sekta ya Elimu, Elimu Msingi (shule ya awali, msingi na sekondari). Ndiyo maana katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minne amefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya shilingi trilioni 5.1 na hiyo kazi inaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepokea pongezi hizo na tunaona hii kazi kubwa ambayo inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita, itaendelea.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?
Supplementary Question 2
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Hezya, Hasanga, Msiya, Kipunga na Kilimampimbi zina upungufu wa walimu wa fizikia na hesabu. Je, ni upi mkakati wa Serikali kutusaidia kutatua tatizo hili? Ahsante sana.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, niaomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali imetoa kibali cha kuajiri walimu 15,925. Mpaka wakati huu walimu 13,105 tayari wameshapangiwa vituo vya kazi katika shule mbalimbali kwenye mamlaka zetu za Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa walimu hawa ambao wataajiriwa katika kibali hiki cha walimu 15,925, wapo walimu wa masomo ya sayansi, ikiwemo fizikia na hisabati. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutaweka kipaumbele kutazama ili tuweze kuleta walimu hao katika Jimbo lake, waweze kutoa elimu nzuri kwa wanafunzi wetu. (Makofi)
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?
Supplementary Question 3
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Changamoto ya upungufu wa Walimu haipo tu Bukene, ipo pia katika Wilaya yetu ya Karatu kwenye shule zetu za msingi na sekondari, hivyo wazazi wanachukua jukumu la kuchanga fedha hili kuwalipa walimu wale wa kujitolea. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba kupitia ajira hizi walimu wanaajiriwa wa kutosha na kuondoa upungufu uliopo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika kuhakikisha kwamba inaendelea kuboresha elimu ya msingi, kwa maana kuanzia shule za awali, madarasa ya awali, msingi na sekondari, inafanya jitihada kubwa sana ya kuongeza walimu kwa sababu udahili wa wanafunzi umeongezeka mara dufu kutokana na utekelezaji wa programu ya elimu bila malipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hatua mahsusi ambazo zinachukuliwa na Serikali ni pamoja na kuajiri Walimu. Kama nilivyotangulia kusema, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa kibali cha kuajiri walimu 15,925. Miongoni mwa walimu hawa wapo walimu wa sayansi ambao watapangiwa vituo vya kazi katika shule mbalimbali kwenye Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Cecilia Paresso kwamba, ninafahamu uhitaji katika Wilaya ya Karatu, katika mgao wa walimu hawa, ninakuhakikishia kwamba Karatu watapatikana walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo fizikia na hisabati, kwa ajili ya kuweza kuwafundisha watoto wetu na kuwapatia elimu iliyo bora. (Makofi)
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Wakati tatizo hili likiisha katika Jimbo la Bukene, bado katika Jimbo la Kishapu kwa maana ya Wilaya ya Kishapu, Kata ya Lagana, Sekondari ya Kiloleli, Sekondari ya Bunambiyu, Sekondari ya Mwamalasa, Mwataga, zina upungufu mkubwa sana wa walimu wa masomo ya sayansi, hasa hisabati, fizikia, baiolojia. Ni lini sasa Serikali itakwenda kutatua tatizo hili ambalo ni kubwa sana katika taaluma, Wilayani kishapu? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ajira za walimu, hizi 15,925 ambazo tayari kuna walimu wameshapangiwa vituo vya kazi, walimu 13,105, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutazingatia uhitaji wa walimu wa masomo haya ya sayansi ikiwemo fizikia, hisabati, pamoja na baiolojia kwenye Jimbo lake na tutaweza kuwapanga walimu hawa ili waweze kuja kuwafundisha watoto katika shule zetu, katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya upungufu wa Walimu wa Masomo ya Hesabu na Physics shule ya Sekondari Bukene?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Manispaa ya Ilemela ina uhitaji wa walimu wa sayansi 325, mpaka sasa tuna walimu 280 wakiwemo na hawa 80 ambao tumepata mgao wa juzi, lakini bado tuna upungufu wa walimu 85 wa sayansi. Je, ni lini sasa tutaongezewa walimu wa sayansi ili waweze kukidhi mahitaji katika shule zetu? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotangulia kusema, kwamba Serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025 imetoa kibali cha kuajiri walimu 15,925, na mpaka wakati huu walimu 13,105 tayari wamepangiwa vituo vya kazi katika shule mbalimbali kwenye Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa. Kwa hiyo, kupitia ajira hizi mpya ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula kwamba, katika shule ambazo ziko kwenye Jimbo lake naye atapata mgao wa walimu hao, wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee vilevile, kutumia nafasi hii kusisitiza mamlaka zetu za Serikali za Mitaa na zenyewe kutumia njia kama kuajiri Walimu kwa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani kwenye Halmashauri, pia kutumia walimu wanaojitolea. Kuna njia nyingi ambazo tunaweza tukazitumia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanapata walimu wa kuwafundisha na tunaweza kupunguza ukali wa upungufu wa walimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutatumia mikakati hii na katika Jimbo lake ataletewa walimu kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo bora. (Makofi)