Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 171 2025-04-29

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya tathmini na kubaini kuwa zinahitajika zaidi ya shilingi bilioni 15 ili kuboresha miundombinu ya Mji wa Katoro, ikiwemo ujenzi wa lami kilometa 10, changarawe kilometa 20 na mitaro kilometa 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza uboreshaji wa miundombinu ya Mji huo kwa kujenga mitaro kilometa nane na ukarabati wa barabara kilometa nane kwa kiwango cha changarawe kupitia Mradi wa Dharura (CERC), kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa mchakato wa ununuzi upo kwenye hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayetekeleza kazi hiyo. (Makofi)