Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 1
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali yanayotia moyo. Ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ni nini mkakati wa Serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwenye Miji Midogo inayokua ya Nyarugusu, Bukoli, Nyakagwe, Chigunga, Nyakagomba, Rwamgasa, Jimboni Busanda?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Waziri yupo tayari kuambatana na mimi kwenda Jimboni Busanda kuona hali ya miundombinu ya barabara hii ninayoizungumzia?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara zetu hizi za Wilaya ambazo zina umuhimu mkubwa sana kiuchumi, lakini zinawawezesha wananchi kufikia huduma za muhimu za kijamii. Ndiyo maana dhamira hiyo utaiona katika ongezeko la bajeti ya TARURA. Mathalani utaona kwenye Wilaya hii, bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.9 mpaka sasa wanapokea shilingi bilioni 5.3 kila mwaka, kwa ajili ya kuhudumia barabara hizi za TARURA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi katika Jimbo lake la Busanda ipo pale pale. Ndiyo maana utaona katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 Serikali imepanga kufanya matengenezo ya barabara kadhaa. Mathalani, Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 166 kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 16 katika Barabara ya Nyamilamba – Nyakagwe, pia Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 148 kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 16 za Barabara ya Bukoli – Nyamigogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imetenga shilingi milioni 248 kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 23 kwenye maeneo ya Rwamgasa na Nyarugusu, vilevile Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 284 kwa ajili ya ukarabati wa kilometa 14 katika Barabara ya Buyagu – Nyarugusu. Ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali kila mwaka wa bajeti inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha inaboresha miundombinu hii ya barabara hizi muhimu ili ziweze kuwanufaisha wananchi. Katika Jimbo la Busanda ninaomba Mheshimiwa Mbunge ninaomba ukae mkao wa kupokea kwa sababu Serikali ya Awamu ya Sita inaleta maboresho makubwa sana katika miundombinu hii muhimu ya barabara. (Makofi)
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 2
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itaboresha barabara za Mji wa Mbalizi kwa kiwango cha lami, ambayo ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano? Ninashukuru sana.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi za Viongozi wetu Wakuu ni kipaumbele namba moja katika mipango na utekelezaji wa shughuli za Serikali. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali italeta fedha katika jimbo lake na katika eneo hili la Mbalizi, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, inafanya maboresho na ukarabati na ujenzi wa barabara muhimu kabisa, hizi alizozitaja Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 3
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Wilaya ya Rungwe, Tukuyu Mjini, kuna Daraja la muhimu sana liitwalo Mafurasopo, daraja hilo ambalo lilibomoka linaunganisha Kata ya Buliaga na Kata ya Ibigi. TAMISEMI kwa kutambua umuhimu wa daraja hilo mlikuja kuangalia na mkasema mtatuma fedha mara moja, ili daraja hilo lijengwe. Sasa je, ni lini daraja hilo la Tukuyu Mjini la Mafurasopo litajengwa? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba, inachukua hatua za dharura kwenye maeneo ambayo mawasiliano yanakatika. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika eneo hili alilolitaja na nitumie pia, fursa hii kuzungumza na meneja wa TARURA wa ngazi ya mkoa na ngazi ya wilaya, waweze kushughulikia maandalizi yote, kwa ajili ya kuchukua hatua za dharura, kwa ajili ya kurudisha mawasiliano katika eneo hili muhimu, ili wananchi waweze kupata miundombinu iliyo bora na wasipate kikwazo cha kufanya shughuli zao za kijamii na za kiuchumi. (Makofi)
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 4
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Ipo Barabara, ya Moo, Kata ya Kimochi, Jimbo la Moshi Vijijini, ambayo inaanzia Barabara ya lami kuelekea Forest na Keys Hotel. Barabara hii ni muhimu kwa sababu, inapita watalii. Ni lini barabara hii itatengenezwa ili iweze kupitika kirahisi? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Felista Njau kwamba, Serikali ina dhamira ya dhati ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara zetu hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Ndiyo maana utaona kila mwaka wa bajeti katika Serikali hii ya Awamu ya Sita bajeti ya TARURA imeongezeka mara dufu kutoka shilingi bilioni 275 kwa mwaka na mpaka sasa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, bajeti ya TARURA itaenda kuwa shilingi trilioni 1.18. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itafika katika maeneo haya aliyoyataja, kwa ajili ya kuimarisha barabara na miundombinu hii, ambayo ina umuhimu mkubwa sana kiuchumi na kijamii pia, kwa wananchi. (Makofi)
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya barabara katika Mji Mdogo wa Katoro ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 5
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Dkt. Samia, alipotembelea Mji wa Babati alitoa ahadi ya kilometa tano za lami na ninaomba nim-quote mwananchi, ambaye amekuwa akiulizia, Mheshimiwa Mbunge kumbushia Bungeni ahadi ya Mheshimiwa Rais ujenzi wa kilometa tano za lami hapa mjini; wananchi wanauliza ni lini ujenzi huo utaanza? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi za Viongozi Wakuu ni kipaumbele namba moja katika utekelezaji wa mipango na majukumu ya Serikali. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Pauline Gekul kwamba, kilometa tano hizo za lami katika jimbo lake zitajengwa. Ninaomba akae katika mkao wa mapokeo, Serikali ya Awamu ya Sita itahakikisha kwamba, fedha zinapatikana, kwa ajili ya kuboresha miundombinu hiyo muhimu kabisa katika jimbo lake.