Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 547 2025-06-10

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuyatambua maeneo yote yanayoathiriwa na maafa na kuweka mkakati wa ziada?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimwa Dorothy George Kilave, Mbunge wa Temeke kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza hatua mbalimbali za kimkakati katika kuyatambua maeneo yaliyoathirika na maafa pamoja na kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu kupunguza athari za maafa hayo kwa kuzingatia Sera ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004, Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 pamoja na miongozo ya kitaifa na kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ambazo Serikali imezichukua ili kutambua maeneo yenye maafa na kupunguza madhara ya maafa hayo ni pamoja na kuandaa Wasifu wa Majanga wa mwaka 2019 ambao umeainisha maeneo yote yaliyo katika hatari; kufanya tathmini ya vihatarishi vya maafa katika Wilaya 36 na kuimairisha mifuko ya ufuatiliaji wa mwenendo wa majanga, ahsante.