Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 172 2025-04-29

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:-

Je, Serikali inatambua biashara ya mtandao na Makampuni mangapi yamejisajili na mapato kiasi gani yamepatikana kwenye biashara hiyo?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI, VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Serikali inatambua uwepo wa Biashara ya Mtandao. Kwa sasa kuna jumla ya kampuni 1,820 ambazo zimesajiliwa, ambapo kampuni 1,075 za Biashara Mtandao ni shughuli yao kuu na kampuni 745 Biashara Mtandao ni shughuli nyingine. Kwa sasa Serikali inaendelea kuchukua hatua muhimu za kuwa na mfumo madhubuti utakaosimamia biashara hiyo ambayo imeanza kuzaa matunda. Mfano, kwa kipindi cha Julai, 2024 hadi Machi, 2025 Serikali ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 192.78 kutoka kwenye Biashara Mtandao, ambayo inajumuisha betting ya mitandaoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuhakikisha tunaenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya teknolojia kwenye biashara, Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Biashara Mtandao (National Electronic Commerce Strategy) ambao upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake. Maeneo yatakayofanyiwa kazi katika utekelezaji wa mkakati huo ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya TEHAMA, uboreshaji wa Sera, Sheria na Kanuni na pia, uboreshaji wa huduma za mawasiliano, usafirishaji na uchukuzi; uimarishaji wa huduma za miamala kwa njia ya mtandao na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu biashara mtandao, ili waweze kutumia mitandao iliyopo kufanya biashara. Ninakushukuru.