Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 173 2025-04-29

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Saranga na Kata ya Mbezi, ambayo Mtaa wa Mpiji Magohe upo, hakuna maeneo yaliyotengwa, kwa ajili ya kujenga Vituo vya Polisi. Napenda kutumia fursa hii kumshauri Mheshimiwa Mbunge, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, kutenga maeneo ili Serikali iweze kujenga Vituo vya Polisi vya Kata ya Saranga na Kata ya Mbezi, ambayo Mtaa wa Mpiji Magohe upo. Ahsante.