Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, wananchi wa Tegeta A, Kata ya Goba, kwa kushirikiana na Mbunge wao, Mheshimiwa Issa Mtemvu, wameweza kujenga Kituo cha Polisi cha Tegeta A na kimefikia kiwango cha 80% ya ujenzi. Je, Serikali ina mpango gani sasa kuhakikisha wanakamilisha kituo hiki, ili wananchi waweze kupata huduma ya ulinzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa, Serikali imeelekeza kwamba, kwa maeneo hayo hatuwezi kupata Vituo vya Polisi kwa sababu, hatuna maeneo. Ninataka kujua, je, Serikali ina mkakati gani wa ziada wa kuhakikisha kwamba, maeneo ambayo hayana Vituo vya Polisi wanawapelekea ulinzi wananchi wake? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mheshimiwa Issa Mtemvu, pamoja na Wananchi wa Tegeta A kwa kazi kubwa uliyoifanya ya ujenzi wa Kituo cha Polisi ambacho kimefikia 80%. Nimhakikishie, Serikali imekuwa ikiunga mkono juhudi za wananchi na katika Kituo cha Tegeta A pia, Serikali itatafuta fedha na kuunga mkono umaliziaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili; ni kweli kuna baadhi ya maeneo bado hawajatenga maeneo, lakini nitoe wito kwa halmashauri zetu kutoa maeneo, kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Polisi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa maeneo ambayo hayana Vituo vya Polisi, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeendelea kulinda raia na mali zao kwa kutumia Vituo vya Polisi vya Jirani. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wilaya ya Tanganyika haina kituo cha Polisi. Mkuu wa Wilaya amefanya jitihada za kuanzisha wadau na kuwapa hadhi ya kuchangia, tumechangia. Ni lini Serikali itaweza kuunga juhudi za Mkuu wa Wilaya na ahadi iliyotolewa na Wizara, shilingi milioni 20 kuwa-support; ni lini Serikali itatekeleza ahadi hiyo? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakoso, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mkuu wa Wilaya kwa hatua hiyo kubwa aliyoanzisha, kuanza kuchanga na kujenga Kituo cha Polisi cha Wilaya. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali kama imeshaahidi shilingi milioni 20 jua ni hela ndogo na nimhakikishie kwamba, tutatafuta fedha hizo na kuziwasilisha, ili wakamilishe Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Tanganyika. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Maswa ni Wilaya Kongwe ya kwanza kabisa katika Mkoa wa Simiyu, haina Kituo cha Polisi. Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi katika Wilaya ya Maswa? Swali hili nimeuliza mara tatu, ni lini watajenga? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Midimu, swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikijenga Vituo vya Polisi vya Makamanda wa Polisi wa Mikoa, Wilaya hata na Kata. Nimhakikishie Mheshimiwa Esther kwamba, swali hili ameshauliza mara nyingi, kituo hiki cha Wilaya ya Maswa kimeshaingizwa kwenye mpango, kitatengewewa fedha na kuanza kujengwa, kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Maswa. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 4

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Momba yenye majimbo mawili ya uchaguzi, Momba pamoja na Tunduma, Kituo cha Polisi chenye hadhi ya wilaya kimejengwa Tunduma, Wilaya ya Momba na Jimbo la Momba hakuna kituo cha Polisi, ambapo Mkuu wa Wilaya anaishi hapo na kuna Police Post tu. Je, ni lini mtatupatia pesa, ili tuweze kujenga Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya kwa kuwa, Mkuu wa Wilaya na vyombo vyake wanaishi hapo? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Condester, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maeneo yote ambayo hakuna Kituo cha Polisi cha Wilaya, amesema kwenye wilaya nzima kuna Kituo kimoja cha Polisi cha Wilaya ila kwa eneo lake la Momba ndio hamna Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya, kwa sasa watumie hicho Kituo cha Polisi cha Kati ambacho kipo maeneo yale, wakati Serikali inajipanga kutafuta fedha, kwa ajili ya kujenga Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya, kwa eneo lake la Momba. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 5

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Ajali za moto zimekuwa zinajitokeza mara kwa mara katika Jimbo la Moshi Vijijini na Askari Zimamoto wamekuwa wanachelewa kufika kutokana na umbali na maeneo ya tukio. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha vituo vya zimamoto katika ngazi ya tarafa ili wananchi waweze kupata huduma? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Profesa Ndakidemi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali, kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, imeendelea kujenga vituo vya zimamoto kwenye mikoa. Mheshimiwa Mbunge ametoa ushauri kwamba, sasa twende kwenye wilaya na tarafa kwa hiyo, ushauri wako umepokelewa pia, utafanyiwa kazi na Serikali. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 6

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Wilaya ya Kalambo haina Jengo la Polisi, wanaazima Majengo ya CCM. Ni lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi, Wilaya ya Kalambo? Ahsante.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bupe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 tumeshatenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kalambo. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 7

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa kushirikiana na Askari tumejenga Kituo cha Polisi, Kata ya Kilando, na kimefikia hatua ya lintel. Nini support ya Serikali, ili angalau kuwaonesha wale Askari walioanza kujitoa, kuwatia moyo basi, kwa kile ambacho kimebakia. (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza la Mheshimiwa Aida Khenani, ambaye leo anauliza kwa mara ya pili, kama sio ya tatu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwanza ninawapongeza sana Askari Polisi ambao wameamua kujenga Kituo cha Polisi, Kata ya Kalando. Nimhakikishie kwamba, Serikali itaunga mkono juhudi hizo nzuri, ili kukamilisha kituo hicho, kwa ajili ya kutoa huduma za wananchi na mali zao. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 8

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Nanyumbu iliahidiwa kujengewa Kituo cha Polisi katika mwaka huu wa fedha ambao unakwisha, bado miezi miwili. Ni lini Kituo hicho cha Polisi kitajengwa?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Mhata, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi ya Serikali ipo palepale, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge. Serikali inatafuta fedha na ikipatikana tutaipeleka, kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu. Ahsante sana.

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 9

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi. Wilaya ya Ludewa inakuwa sana kwa shughuli za kiuchumi na kijamii na kumekuwa na matukio ya moto, hasa kwenye mabweni. Nini mpango wa Serikali kuleta gari la zimamoto Ludewa?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshaagiza magari na imeshalipia magari 150 ya Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya kusambaza katika wilaya zote hapa nchini ikiwepo na Wilaya ya Ludewa. (Makofi)

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi Mitaa ya Mpiji Magohe na Saranga katika Jimbo la Kibamba?

Supplementary Question 10

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Je, ni upi mpango wa Serikali wa kukarabati nyumba za polisi zilizopo Kata ya Kiusa, Manispaa ya Moshi ambazo zinavuja sana? Swali hili nimeshaliuliza tena hapa Bungeni.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru na ninaomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bushiri, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za askari wake wote hapa nchini pamoja na magereza. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pia kwamba eneo la Moshi ambalo amelisema tutaliweka kwenye mpango na kulitafutia fedha kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hizo ili askari wake katika maeneo salama waendelee kulinda raia na mali zao. Ahsante sana.