Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 174 2025-04-29

Name

Maulid Saleh Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka utaratibu wa kujenga Vituo vya Polisi daraja C Katika kila Kata na Shehia hapa nchini. Katika Shehia ya Mtofani Jimbo la Welezo Zanzibar hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi. Ninaomba nitoe wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Magharibi A kutenga eneo, ili Serikali iweze kujenga kituo cha Polisi katika Shehia ya Mtofani. Ahsante. (Makofi)