Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maulid Saleh Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. MAULID SALEHE ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza. Je, ni lini Serikali itaweka mkakati wa kuwa na database ya pamoja ya ukusanyaji wa taarifa na utunzaji wa kumbukumbu na upokeaji wa malalamiko ya wananchi kwenye vituo vya polisi nchini?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Salehe Ali, Mbunge wa Welezo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tayari ina mfumo thabiti kabisa wa kupokea na kutunza kumbukumbu au malalamiko ya wananchi. Hili kwa sasa limeanzia kwenye Ofisi za Mikoa yote kwa Makamanda wa Mikoa na Makao Makuu. Mpango ni kuhakikisha kwamba mfumo unaendelea kwenye wilaya na vituo vidogo vya chini. Ahsante sana.

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 2

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa Kijiji cha Pujini kuna kiwanja cha kujengea kituo cha polisi. Je, ni lini Serikali itajenga kituo hicho cha polisi kilichopo Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Maryam kwa ufuatiliaji wake. Nimhakikishie kwamba, kuwa eneo tayari wameshalitenga Serikali pia itatenga fedha kwa ajili ya Kituo cha Polisi kule Chake Chake Pemba. (Makofi)

Name

Rashid Abdalla Rashid

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiwani

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 3

MHE. RASHID ABDALLA RASHID: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itakamilisha Kituo cha Polisi Jamii, Shehia ya Kendwa ambacho wananchi wenyewe wamekwishakamilisha hadi hatua ya linta? Ahsante.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Rashid Abdalla, Mbunge wa Kiwani, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli na nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, amekuwa akifuatilia sana na juzi nilikuwa naye Ofisini kwangu tumelizungumzia jambo hili. Nimhakikishie kama nilivyomwahidi, kwamba Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo cha polisi ambacho kimejengwa na wananchi na nimpongeze kwa kazi kubwa anayoifanya. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 4

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi katika Tarafa ya Daudi kama ilivyowekwa kwenye mpango wa bajeti mwaka huu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Kituo cha Polisi cha Daudi tupo kwenye mpango na tunatafuta fedha, zikishapatikana tutazipeleka kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho tayari kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Tarafa ya Daudi pamoja na Wilaya ya Mbulu.

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 5

MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa Serikali itajenga Kituo cha Polisi Makao Makuu ya Halmashauri kwa kuwa tayari Mkurugenzi ameshatoa eneo na mimi Mbunge nimechangia tofali 5,000. Sasa nini commitment ya Naibu Waziri ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo? Ahsante sana.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Iddi Iddi, Mbunge wa Msalala, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na pia Halmashauri kwa kutenga eneo tayari kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya. Nimhakikishie, kwamba Serikali hii sikivu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inayojali usalama wa raia na mali zao itatenge fedha kwa ajili ya kujenga Kituo cha Polisi cha Wilaya kule Halmashauri ya Msalala. Ahsante sana.

Name

Juma Usonge Hamad

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chaani

Primary Question

MHE. MAULID SALEHE ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi Shehia ya Mtofani katika Jimbo la Welezo Zanzibar?

Supplementary Question 6

MHE. JUMA USONGE HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Takribani zaidi ya miaka mitatu ninaulizia na ninakililia Kituo changu cha Polisi kilichopo Jimbo langu la Chaani, Lungalunga. Je, ni lini Serikali italeta ile shilingi milioni 80 waliyoahidi mwaka jana kwenye mwaka wa bajeti kwa ajili ya kukimalizia Kituo cha Polisi kilichopo Lungalunga?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Usonge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali iliahidi kupeleka shilingi milioni 80 kwa ajili ya kumalizia kituo cha polisi alichokitaja, cha eneo la Chaani. Nimhakikishie kwamba mwaka wa fedha unaendelea tutahakikisha kwamba tunapata fedha kwa ajili ya kukamilisha kituo cha polisi ambacho kipo hatua nzuri. Ninashukuru sana.