Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 14 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 175 | 2025-04-29 |
Name
Kenneth Ernest Nollo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:-
Je, lini Serikali italeta Muswada kuhakikisha Mfuko wa Taifa wa Maji unakuwa na chanzo cha uhakika cha fedha za Mfuko huo?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo cha uhakika cha fedha kwa Mfuko wa Taifa wa Maji kwa sasa ni tozo ya Shilingi 50 inayotokana na mauzo ya mafuta ya dizeli na petroli. Aidha, pamoja na kuwepo kwa chanzo hicho, Serikali imeendelea kubuni vyanzo vingine vya kutunisha Mfuko huo ikiwemo uwekezaji wa hati fungani na uandaaji wa maandiko ya miradi ili kupata fedha kutoka katika Mifuko ya Kimataifa ya kufadhili utekelezaji wa miradi ya maji, ambapo kiasi cha Dola za Marekani milioni 17.35 zimepatikana kupitia Dirisha la Mabadiliko ya Tabianchi la Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutafuta vyanzo vingi zaidi kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa fedha kwa Mfuko wa Taifa wa Maji ili uweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved