Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali italeta Muswada kuhakikisha Mfuko wa Taifa wa Maji unakuwa na chanzo cha uhakika cha fedha za Mfuko huo?

Supplementary Question 1

MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Swali la kwanza; Mfuko huu unakusanya takriban shilingi bilioni 250 na zaidi, lakini Serikali imeweka ukomo wa bajeti kwenye Mfuko huu wa shilingi bilioni180. Sasa kutokana na matatizo mkubwa ya maji kwa nini, Serikali inaweka ukomo wa bajeti kwenye fedha zile ambazo ni fedha maalum kwa ajili ya Mfuko ule? Serikali inatafuta vyanzo vingine kuongeza fedha wakati fedha inazokusanya imeweka cut off point haizitumii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; mwaka jana katika Kata yangu ya Chali takribani watu 14 walifariki kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa ukosefu wa maji. Upo mradi pale unaendelea Serikali imelipa mkandarasi lakini kazi ya kuendeleza hatua inayofuata haifanyiki Serikali ina mpango gani wa kukamilisha mradi huu wa maji katika Kata ya Chali ambao umechukua miaka mitatu sasa pila mafanikio?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na kumshukuru Mheshimiwa Kenneth Nollo, Mbunge wa Bahi kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kwa ufuatiliaji wa miradi ndani ya jimbo lake na vilevile kwa ushauri ambao ameendelea kutupatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maji tunatambua Mfuko wetu wa Maji ni mfuko ambao upo kwa mujibu wa sheria kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema. Vilevile tunatambua kwamba sisi Wizara ya Maji tumeendelea kushirikiana na wenzetu Wizara ya Fedha; na kwa kweli tangu tumeenza kuongea nao tumeona mtiririko wa fedha umeendelea kuboreshwa zaidi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeenda zaidi ya hapo, Mfuko wa Maji umeingia MOU na TRA ili tuwe na uhakika kwamba kile kinachokusanywa ndicho ambacho kinakuja. Kwa kweli tumeona kwamba kuna improvement kubwa. Nimhakikishie tu pamoja na Bunge lako Tukufu, kwamba changamoto ambazo bado zipo katika namna ambayo ceiling inavyowekwa tupo katika mazungumzo na tupo katika hatua nzuri. Kwa hiyo hilo tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, nikiri kabisa, kwamba Mradi wa Chali, Igongo Isanga pamoja na eneo la Makulu ni mradi ambao unagharimu shilingi bilioni 2.5. Ninatambua pia mkandarasi alikuwa anatudai 1.5 na Serikali imekwishamlipa. Sisi tumekwishaelekeza, kwamba mkandarasi asiporudi site na kuendelea na kazi DG RUWASA ahakikishe kwamba kwa kutumia wataalam wake wa kisheria aletwe katika meza na atuambie kwa nini harudi. Ikibainika kwamba hana nia njema na mradi ule basi Serikali itachukua hatua stahiki za kisheria ili ku-terminate kabisa ule mkataba na wengine wapatikane kwa ajili ya kuutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelewa kabisa kwamba Serikali inaendelea kuwekeza katika eneo la Bahi na tuna visima tunaendelea kuchimba katika eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge anatamani mradi ukamilike ili kuhakikisha kwamba tunaendelea subsidize maeneo ambayo bado yana changamoto kubwa ya maji. Ninakushukuru sana.