Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Water and Irrigation Wizara ya Maji 176 2025-04-29

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Je, lini Awamu ya Pili ya Mradi wa Maji wa Rutunguru, Kaisho - Isingiro utaanza ili kuondoa adha wanayoipata wananchi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Maji Kaisho-Isingiro ambayo inahusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa maji lita 225,000 pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 17. Lengo la mradi huo ni kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 37,500 waishio kwenye vijiji 11 vya Kaisho, Nyabishenge, Ibare, Ishaka, Karukwanzi A, Karukwanzi B, Kihanga, Kaitambuzi, Katera, Rutunguru pamoja na Nyakakoni. Utekelezaji wa awamu hiyo umefikia 95% na unatarajia kukamilika mwezi Juni, 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inaendelea kutatafuta fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi huo. Ahsante.