Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, lini Awamu ya Pili ya Mradi wa Maji wa Rutunguru, Kaisho - Isingiro utaanza ili kuondoa adha wanayoipata wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Miradi ya Maji ya Runyinya, Chanya, Kikukuru, Kimuli, Rwanyango wakandarasi wameondoka site kwa sababu hamna certificate. Ningependa kujua, je, ni lini Serikali itawalipa ili waweze kukamilisha mradi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; Mradi wa Maji Nyakanazi, Biharamulo umesimama kutokana na madai ya mkandarasi. Je, ni lini mkandarasi atalipwa pesa hiyo ili naye aweze kukamilisha mradi huo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na nimshukuru sana Mheshimiwa Oliver Semuguruka pamoja na Mbunge wa eneo husika kwa kuendelea kuwapigania wananchi wa Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Nyakanazi, Biharamulo ni mradi ambao unatekelezwa na mkandarasi Bozz Bona ambapo chanzo tayari kilishajengwa, tenki limeshajengwa, na bomba zimeshalazwa. Hata hivyo, tunaelewa kwamba kuna sehemu chache na DP hazijakamilika. Tunatambua kwamba mkandarasi huyo anatudai na Serikali inayafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa pili ni upande wa mradi wa Kikukuru mradi huu wenye gharama ya shilingi bilioni 5.1 ambao unatekelezwa na mkandarasi wa Tondwe umefikia 92%; kwenye upande wa chanzo alikuwepo mkandarasi mwingine anaitwa Serengeti ambaye ameomba ku-withdraw yeye mwenyewe ili asiendelee na mradi huo. Sasa Serikali imeanza utaratibu wa kuhakikisha kwamba tunapata mkandarasi mwingine ili aweze kumalizia upande wa chanzo ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, lini Awamu ya Pili ya Mradi wa Maji wa Rutunguru, Kaisho - Isingiro utaanza ili kuondoa adha wanayoipata wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Vijiji vya Kitanula, Kalangali, Ipalalyu, Itagata na Mbugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi havina kabisa mtandao wa maji. Je, upi mkakati wa Serikali wa kupeleka maji katika vijiji hivyo ili kumtua ndoo mwanamke? Ninakushukuru.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri ya kuwapambania Wanasingida.

Mheshimiwa Mwenyekiti katika maeneo haya tumechimba visima vitano, lakini kuna visima vitatu bahati mbaya hatujafanikiwa kupata maji. Tunaendelea kufanya utafiti ili tuweze kuona tunatatua changamoto hii kwa namna ambayo itafaa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametenga kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vijiji ambavyo havina maji vihakikishe kwamba tunawapelekea miradi ya maji, ukiwemo Mradi mkubwa wa Miji 28 ambao unagharimu shilingi bilioni 17. Kwa sababu lile tenki limejengwa mpakani kati ya Manyoni Mashariki na Manyoni Magharibi, yaani Itigi. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba tutakapokuwa tumejiridhisha kuwa hatujapata chanzo kingine basi tenki hilo litasaidie kupeleka upande wa Itigi na kutatua changamoto ya maji katika maeneo haya. Ahsante sana. (Makofi)