Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 177 2025-04-29

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-

Je, lini Serikali itafuta Hati ya Shamba la Balali na kuwakabidhi wananchi wa Melela?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mgogoro wa Shamba la Balali kwa muda mrefu ulikuwa ukishughulikiwa na Serikali ili kuweza kuutatua kiutawala. Hata hivyo, wananchi waliokuwa wanalalamikia shamba hili waliamua kutumia njia ya Mahakama kwa kufungua shauri Mahakama Kuu. Baada ya Mahakama kusikiliza hoja za wananchi hao pamoja na mmiliki wa shamba iliamua kuwa shamba tajwa ni mali ya familia ya Balali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huu ulishughulikiwa na Mahakama Kuu Mkoa wa Morogoro kupitia Shauri la Ardhi Na.5 la mwaka 2023. Natoa rai kwa wananchi kuheshimu uamuzi uliotolewa na Mhimili wa Mahakama.