Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Serikali itafuta Hati ya Shamba la Balali na kuwakabidhi wananchi wa Melela?

Supplementary Question 1

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; mgogoro huu wa Shamba la Balali unafanana kabisa na mgogoro wa Shamba la Kambenga. Je, Serikali ina mpango gani katika kuutatua mgogoro wa Kambenga?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana jioni nimepokea wananchi kutoka Kijiji cha Utengule wakiambatana na Mwenyekiti wao wa Kijiji kuna mgogoro baina ya Kitalu cha uwindaji na wananchi wa Kijiji cha Utengule. Je, yupo tayari mara tu baada ya kipindi hiki cha Bunge nimkutanishe na hao wananchi niliowapokea jana?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana naye kwamba mara baada ya kipindi hiki cha maswali tukutane ili kuweze kujadili mambo yote haya mawili.