Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 178 2025-04-29

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete Tabora?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Kitete unatekelezwa kwa awamu ambapo hadi sasa Serikali imetoa fedha shilingi bilioni 3.27 ambapo awamu ya kwanza zilitolewa shilingi bilioni 2.69 na awamu ya pili shilingi milioni 578.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka huu wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete ambapo hadi sasa ujenzi umefikia 50%. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari, 2026.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.