Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 548 2025-06-10

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Same ni miongoni mwa wilaya ambazo zina mtandao wa barabara zilizoko sehemu za milimani kwenye Tarafa za Mamba, Vunta, Gonja, Chome Suji, Ndungu na Mwembe Mbaga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa Serikali imekwisha jenga barabara za zege zenye urefu wa mita 5,692 kwa gharama ya shilingi bilioni 3.87 katika Barabara za Hedaru – Vunta – Myamba, Mpirani Dispensary – Dindimo Primary School, Maore – Vuje, Maore – Kalungoywo, Msanga – Chome, Hedaru – Makasa, Saweni – Gavao, Ndungu – Lugulu, Kisiwani – Msindo na Suji – Mweteni katika maeneo yenye kona hatarishi za mlima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2025/2026 Serikali imeweka katika mipango yake ujenzi wa barabara za zege zenye urefu wa mita 530 katika Barabara za Bombo – Mpirani, Kizangaze – Mtii, Hedaru – Vunta, Idaru – Narema, Mbuyuni – Marindi na Manka – Madiveni kwa gharama ya shilingi milioni 360.39.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuhudumia barabara na madaraja Wilayani Same kwa kujenga, kukarabati na matengenezo zikiwemo barabara zenye tabaka la zege kulingana na upatikanaji wa fedha.