Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 1
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana ambayo yanatia moyo. Ninashukuru sana kwamba kwenye sehemu hizi za barabara zilizotiwa zege zimeboresha sana usafiri katika kata tajwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu ni kwamba; je, kwa kuwa mitaro iliyojengwa pembezoni mwa hizi barabara ziizotiwa zege, mvua ikinyesha madongo na takataka zinaangukia pale inaziba na kutembea na barabara na kuharibu yale maeneo ambayo hayajatiwa zege.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuunda kikosi kazi cha vijana ili waweze kuwa wanahudumia hizi barabara wakati TARURA labda hajaweza kufanya kazi hiyo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa adui namba moja wa barabara zetu hizi ni maji na hasa sasa hivi Serikali imejielekeza katika kujenga barabara pamoja na miundombinu ya mitaro, lengo ikiwa ni ku-drain yale maji ili yasiharibu barabara. Sasa kuna mazingira ambayo inatokea kwamba ile mitaro inajaa takataka na lile lengo la kujengwa mitaro ile linapotea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI imebuni mradi mahususi kabisa kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa ajili ya kuunda vikundi vya kijamii ambavyo vitakuwa na kazi mahsusi kabisa ya kufanya matengenezo madogo pamoja na kufanya usafi wa barabara zetu ikiwa ni sehemu mojawapo kwanza ya kuwasaidia vijana na haya makundi ya kijamii kupata ajira, lakini pia ikiwa ni mkakati mahususi kabisa wa kuhakikisha barabara zinazojengwa na Serikali zinaishi kwa muda uliopangwa wa kutengenezewa mazingira ya kuwa bora zaidi na kuondoa mazingira ya uchafu kwenye mitaro, lakini maji kutwama kwenye barabara na kuziharibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali kupitia mradi huu ambao unaitwa CDRM Component of the RISE Project ambao huu mradi upo chini ya Benki ya Dunia kwa kushirikiana na ILO Serikali imeshaanza kufanya majaribio katika baadhi ya halmashauri, lakini lengo mradi huu ufike katika maeneo yote Tanzania kuhakikisha kwamba barabara zetu zinalindwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa zina jukumu la msingi la kuhakikisha inafanya usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Kwa hiyo, pia nitumie nafasi hii kuendelea kuwakumbusha Wakurugenzi wote katika Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa kutimiza wajibu wao wa msingi wa kutengeneza mazingira ya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na usafi katika maeneo ya miundombinu hii ya mitaro ili kuepusha mazingira ya mitaro kujaa na barabara mwisho wa siku kuharibika japokuwa miundombinu hii ya ku-drain maji tayari inakuwa imetengenezwa. (Makofi)
Name
Christopher Olonyokie Ole-Sendeka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Simanjiro
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 2
MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Kwa kuwa Barabara ya Msitu wa Tembo kwenda Ngorika imejengwa na TARURA kwa kujenga tuta la kilometa mbili na kuweka lami juu sasa na kujenga madaraja; je, Serikali inasema nini kuhusu kujenga barabara hiyo kilometa kumi zilizokuwa zimeahidiwa kujengwa kwa barabara ya lami ili kuweza kuwezesha eneo hilo liweze kupitwa kwa uhakika? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara zetu hizi zinazosimamiwa na TARURA yaani barabara za wilaya na ndio maana utaona kwamba kila mwaka wa bajeti fedha zinaendelea kuongezwa katika upande huu wa kuhudumia barabara hizi za TARURA. Tunazungumza mwaka 2020/2021 bajeti ya TARURA ilikuwa ni shilingi bilioni 275 lakini muda huu tunavyozungumza katika mwaka wa bajeti 2025/2026 tunatarajia bajeti ya TARURA itakuwa ni shilingi trilioni 1.18.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ongezeko la bajeti hii ya TARURA linaonekana hata katika wilaya zetu. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Ole-Sendeka kwamba Serikali kwa kuwa tayari imeshaanza kujenga hii kilometa mbili katika Barabara ya Msitu wa Tembo kwenda Ngorika, nimhakikishie hata hii kilometa kumi nyngine ya lami iliyobakia Serikali itafika, ili ihakikishe inaiboresha barabara hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi katika shughuli zao za kiuchumi, pia katika kufikia huduma za msingi za kijamii. (Makofi)
Name
Joseph Kasheku Musukuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, barabara inayotoka Kijiji cha Bweya kilichopo Kata ya Rwezela kwenye Jimbo la Geita haipitiki kabisa kwa sasa, si kwa gari, si kwa pikipiki. Barabara hiyo haikuwemo kwenye bajeti kwa sababu ilipewa fedha na TASAF kama shilingi milioni 60.
Mheshimiwa Mwenyekti, kutokana na mafuriko yaliyojitokeza kwenye Jimbo la Geita, barabara hii imeharibika kwa kiasi kikubwa na tathmini ya TARURA imetoka kama milioni 130. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri unatamka nini kuhusu kuiongezea fedha ya dharura barabara hiyo ili iweze kutengenezwa watoto waweze kupita kwenda shule? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuna mazingira ambayo barabara zetu hizi za TARURA zinakatika mawasiliano yaani mawasiliano yanakatika kutoka eneo moja kwenda linguine na ndio maana Serikali inatenga bajeti ya dharura. Katika mwaka wa bajeti huu tuliokuwa nao bajeti ya dharura ni shilingi bilioni 71 na Bunge hili lilipitisha nyongeza ya bajeti ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuhudumia eneo hili la barabara hizi ambazo zinaharibika kwa mazingira ya dharura.
Kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumuagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa akishirikiana na Meneja wa TARURA wa Wilaya waweze kuifikia barabara hii aliyoitaja Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma na kuifanyia tathmini na walete maombi Ofisi ya Rais - TAMISEMI walete huku kwa Chief wa TARURA, ili tuiweke katika mipango ya kuifikia na kuihudumia kwa dharura.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 4
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara kutoka Lundugai kwenda Kambi ya Chokaa - Simanjiro kwa Mzee Sendeka hapa, haipitiki kwa sasa na hivyo mawasiliano kati ya Wilaya ya Hai na Simanjiro ni kama yamekatika kabisa.
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara hii muhimu ya kuunganisha wilaya hizi mbili? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatammbua mazingira ambayo yanajitokeza ambapo maeneo yanaathirika na mawasiliano yanakatika kutokana na mazingira ya mvua na hali nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie nafasi hii kumuagiza Meneja wa TARURA wa Kilimanjaro akishirikiana na wa Manyara pamoja na Mameneja wa Wilaya hizi mbili wahakikishe kwamba wanafanya tathmini katika eneo hili alilolitaja Mheshimiwa Saashisha Mafuwe na waweze kuleta maombi ya fedha kwa ajili ya kuja kuchukua hatua za kidharura za kurudisha mawasiliano katika barabara hii ambayo inaunganisha Wilaya mbili za Hai na Simanjiro. (Makofi)
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 5
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana, pale kwetu Igunga kuna mkandarasi amesaini mkataba Barabara ya kutoka Igunga Mjini kwenda Mwanzugi, itumba, Lugubu mpaka njia panda ya kule Nsimbo, lakini mpaka sasa zaidi ya miezi mitatu mkandarasi hajaingia site lakini ameshasaini mkataba.
Nini kauli ya Serikali kupitia TAMISEMI na TARURA kuhakikisha mkandarasi huyu anaingia site, ili aweze kutoa huduma kwa wananchi hususan ukanda huu ambao unazalisha Kilimo cha Mpunga kwa wingi? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (NHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kabisa Serikali ya Awamu ya Sita lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba, inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara zetu hizi za TARURA, lakini kikubwa zaidi kwa maenelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, amekuwa akisisitiza kwamba wakandarasi pindi wanapokuwa wametia saini katika mikataba kwa ajili ya kufanya kazi hizi za ujenzi wa barabara, basi waweze kusimamia makubaliano yale ambayo yapo katika mkataba ya kutekeleza mradi husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Tabora, lakini na Meneja wa TARURA wa Wilaya, waweze kuniletea taarifa ya kwa nini mkandarasi huyu ambaye ametia saini katika mkataba wa ujenzi wa barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge bado hajafika site na hajaanza kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo ni kuhakikisha kwamba mkandarasi huyu anatimiza wajibu kwa mujibu wa mkataba. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge tutafuatilia suala hili mimi na wewe, nitakupa mrejesho. (Makofi)
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga barabara za vijijini zilizopo milimani - Same kwa mawe au zege ili kupunguza gharama za kufanya matengenezo?
Supplementary Question 6
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Barabara ya Rukuraijo kwenda Kitwechenkura mpaka kuunganisha Kata ya Songambele tumeiandikia muda mrefu; ni lini barabara hii itajengwa ili ipitike vizuri?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuimarisha barabara zetu hizi muhimu kabisa za TARURA, barabara za wilaya ambazo zina umuhimu mkubwa katika kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi, lakini kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na utaiona dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha barabara hizi kwa ongezeko la Bajeti na hizo bajeti siyo tu bajeti kwa ujumla wake, lakini inaonekana hata katika ongezeko la bajeti katika kila wilaya.
Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Bilakwate kwamba katika barabara aliyoitaja dhamira ya Serikali ni kuifikia. Serikali itaifikia barabara hii ili iweze kuijenga na iweze kuwanufaisha wananchi wako.